ZAHANATI YA NJELENJE MBEYA LAWAMANI
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi
...................................................................................................
LUGHA za manyanyaso ambazo
zinatumika na wauguzi wa Zahanati ya Njelenje Wilaya ya Mbeya zimewafanya
wanawake wa kijiji hicho kuamua
kujifungulia majumbani kwao ili kukwepa matusi wanayotukanwa.
endelea.....
Hata hivyo wanawake hao licha ya kuamua kujifungulia
majumbani mara baada ya kupata nguvu hufika katika zahanati hiyo kupata kinga
za watoto ambako wauguzi hao huwapiga faini tena ya sh.5000 kwa kosa kuhoji kwanini wamejifungulia nyumbani.
Katika utafiti wa mtandao huu uliofanywa kwa muda wa wiki moja kwa kushirikiana na
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umebaini kuwa fedha ambazo wanatozwa akina
mama hao ni sehemu kipato ambacho wameanzisha wauguzi hao kwa manufaa yao
binafsi.
Hata hivyo wanawake ambao wamekuwa waqkijifungulia majumbani
ni wale ambao wanatoka vijiji vya
Iwola,Ilea ndo hujifungulia nyumbani
ambako hata umbali nao unachangia
kwa wanawake hao.
Akizungumza na Mtandao huu Bi.Edina Mgata mkazi wa Iwola
alisema kuwa kujingulia nyumbani kwao ni kawaida kwani lugha chafu wanazopewa
na manesi wanaona ni vema wasifike hospitali kujifungulia.
“Muda mwingine mwanamke anashikwa na uchungu usiku pindi anapofika katika zahanati hiyo
kunakuwa kumefungwa hivyo mgonjwa kuamua kwenda nyumbani kwa Muuguzi kugonga
hujibiwa kuwa anasumbuliwa na mgonjwa
kuendelea kusubiri mpaka anajifungua peke yake kutokana na nesi kuamka kwa kujilazimisha huku mgonjwa
akiwa hajiwezi”alisema.
Diwani wa kata ya Mshewe Bw. Fabian Mwakasole baada ya
kuulizwa na mwandishi wa habari hizi alikana kutokuwepo kwa malalamiko hayo
toka wanawake hao na kuhaidi kufika
katika zahanati hiyo ili kubaini ukweli uliopo.
“Unajua wananchi wakiona wageni wanapenda sdana kuongea
pasipo kujua anayeongea nae ni nani ,wananchi wangu nawajua nitafatilia suala
hili kwa undani kujua”alisema Diwani huyo.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Njelenje
Bw.Emmanuel Kalimoja alisema kuwa hana taarifa ya malalamiko hayo kutoka kwa
wanawake hao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment