MANISPAA YA IRINGA YAMALIZA UTATA KATI YA MACHINGA NA POLISI ENEO LA MASHINE TATU YAGEUZA STENDI YA DALADALA
Daladala zikiwa zikisubiri abiria
katika stendi mpya ya Mashine tatu katika Manispaa ya Iringa eneo
ambalo awali machinga walikuwa wakilitaka kwa shughuli zao siku za
jumapili
Na Meck Lameck
endelea.....
Hili ndilo eneo maarufu la kihistoria katika mji wa Iringa eneo la Mashine tatu
| Daladala zikiwa katika stendi mpya ya soko la Mashine tatu na chini ni picha za maktaba yetu jinsi hali ilivyokuwa awali |
Mbunge Msigwa akiondoka eneo la mashine tatu
Machinga wakisukuma gari ya mbunge Msigwa
Polisi wakimfuatilia mbunge Msigwa kwa nyuma baada ya kufika eneo hilo bila kufanya biashara kama alivyoahidi
HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa
mkoani Iringa imefanikiwa kumaliza utata uliokuwepo kati ya
wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) na polisi baada ya kuligeuza
eneo lililokuwa likigombewa na machinga eneo la mashine tatu kuwa
stendi ya daladala zinazofanya safari zake nje ya mji wa Iringa .
Mtandao huu wa matukiodaima.com
umetembelea eneo hilo na kushuhudia eneo hilo likiwa tulivu kwa
sasa baada ya kugeuzwa kuwa eneo la stendi ya daladala .
Wakizungumzia hatua hiyo ya uongozi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kugeuza eneo hilo kuwa stendi
ya daladala Bw Omari All na Kevin Sanga ambao ni machinga mjini
Iringa mbali ya kupongeza hatua hiyo ambayo wamedai imeipusha
machafuko zaidi ila bado wameomba uongozi wa Manispaa ya Iringa
kuwaboreshea eneo la Mlandege ambalo wanaendelea kulitumia kwa
shughuli za gulio kila jumapili.
Kwa walisema kuwa eneo hilo la
mashine tatu ambalo sasa limefanywa stendi ya daladala lilikuwa ni
zuri zaidi kwao kiuchumi ila kwa kuwa serikali iliwataka
kuondoka eneo hilo hawanapingamizi na uamuzi huo wenye sura ya
kuuweka mji katika mpangilio mzuri zaidi.
"Sisi hatuna pingamizi lolote na
uamuzi wa Manispaa kugeuza eneo hili stendi ya daladala ila bado
tunaomba kuboreshewa mazingira ya gulio la Mlandege ama kupewa eneo
la barabara mbili kwa siku za jumapili"
Huku Madereva wa daladala katika
stendi hiyo wakidai kuwa eneo hilo awali ilikuwa ni gumu kujulikana
kwa abiria ila kwa sasa wananchi wengi wamelitambua hivyo hakuna
tatizo lolote kwao.
No comments:
Post a Comment