Mugabe ‘amburuta’ Tsvangirai
Vyama vinavyochuana ni pamoja na Zanu-PF cha Mugabe, MDC kilichomsimamisha Tsvangirai. Vingine ni Independent, UPP na Zapu.
Endelea...
Endelea...
Vyanzo mbalimbali vya habari vinaonyesha kuwa
Mugabe amemwacha mpinzani wake kwa asilimia nyingi na zaidi katika jiji
la Harare na Bulawayo.
Mugabe atamba
Akizungumza kwa kujiamini huku akiwa na wafuasi wake kadhaa, Mugabe alisema ana uhakika wa kupata ushindi wa kishindo.
Aliliambia Shirika la Habari la Uingereza
(Reuters): “Sioni sababu ya kunifanya niwe na wasiwasi… hakuna
kitakachonifanya nishindwe katika uchaguzi huu.”
Hata hivyo, Mugabe aliyeiongoza Zimbabwe tangu
uhuru 1980, alisema iwapo atashindwa, yuko tayari kukabidhi madaraka kwa
amani… “Ninaweza kustaafu baada ya kuwa madarakani kwa miaka 33 iwapo
nitashindwa katika uchaguzi huu,” alisema.
Akizungumza baada ya kupiga kura juzi, Mugabe
alisema ana uhakika kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki, kwa
kuwa wagombea wote walipewa nafasi ya kutosha kufanya kampeni na
wananchi kushiriki katika uchaguzi huo.
Alipoulizwa iwapo ana shaka yoyote kuhusiana na
matokeo, alicheka kwa kejeli na kusema hawezi kuwa na hofu katika mambo
ambayo amekutana nayo kwenye maisha yake na kuyashinda, akiwa na umri wa
miaka 89 sasa.
Kumekuwa na taarifa zisizo rasmi kwamba iwapo
Mugabe atashinda, anatarajia kustaafu kabla ya sherehe yake ya miaka 90
ya kuzaliwa na kumwachia madaraka mshirika wake ndani ya Zanu-PF.
Lakini alipoulizwa iwapo ataweza kuhudumu kwa
kipindi cha miaka mitano, alisema: “Kwa nini isiwe? Hamtaki nihudumu kwa
kipindi chote? Kwa nini nijitolee kuwa mgombea kwa ajili ya
kuwadanganya watu kama nisingekuwa na mpango wa kuwatumikia?”
No comments:
Post a Comment