Pages

Thursday, 15 August 2013

ZAHANATI YA NJELENJE MBEYA LAWAMANI

 
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Ali Mwinyi
...................................................................................................

LUGHA za  manyanyaso ambazo zinatumika na wauguzi wa Zahanati ya Njelenje Wilaya ya Mbeya zimewafanya wanawake wa kijiji  hicho kuamua kujifungulia majumbani kwao ili kukwepa matusi wanayotukanwa. 
endelea.....
Hata hivyo wanawake hao licha ya kuamua kujifungulia majumbani mara baada ya kupata nguvu hufika katika zahanati hiyo kupata kinga za watoto ambako wauguzi hao huwapiga faini tena ya sh.5000 kwa kosa  kuhoji kwanini wamejifungulia  nyumbani.
Katika utafiti  wa mtandao huu uliofanywa  kwa muda wa wiki moja kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umebaini kuwa fedha ambazo wanatozwa akina mama hao ni sehemu kipato ambacho wameanzisha wauguzi hao kwa manufaa yao binafsi.
Hata hivyo wanawake ambao wamekuwa waqkijifungulia majumbani ni wale ambao wanatoka vijiji  vya Iwola,Ilea ndo hujifungulia nyumbani  ambako hata umbali  nao unachangia kwa wanawake hao.
Akizungumza na Mtandao huu Bi.Edina Mgata mkazi wa Iwola alisema kuwa kujingulia nyumbani kwao ni kawaida kwani lugha chafu wanazopewa na manesi wanaona ni vema wasifike hospitali kujifungulia.
“Muda mwingine mwanamke anashikwa na uchungu  usiku pindi anapofika katika zahanati hiyo kunakuwa kumefungwa hivyo mgonjwa kuamua kwenda nyumbani kwa Muuguzi kugonga hujibiwa kuwa anasumbuliwa na  mgonjwa kuendelea kusubiri mpaka anajifungua peke yake kutokana na  nesi kuamka kwa kujilazimisha huku mgonjwa akiwa hajiwezi”alisema.
Diwani wa kata ya Mshewe Bw. Fabian Mwakasole baada ya kuulizwa na mwandishi wa habari hizi alikana kutokuwepo kwa malalamiko hayo toka wanawake hao  na kuhaidi kufika katika zahanati hiyo ili kubaini ukweli uliopo.
“Unajua wananchi wakiona wageni wanapenda sdana kuongea pasipo kujua anayeongea nae ni nani ,wananchi wangu nawajua nitafatilia suala hili kwa undani kujua”alisema Diwani huyo.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Njelenje Bw.Emmanuel Kalimoja alisema kuwa hana taarifa ya malalamiko hayo kutoka kwa wanawake hao.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment