Pages

Thursday, 12 December 2013

Jeshi la Polisi Singida laua majambazi wawili

WADAU TUNAOMBA RADHI KWA TASWIRA HII KAMA ITAKUKWAZA.
DSC04892
WATU wawili wakazi wa manispaa ya Singida ambao majina yao bado hayajajulikana,wakiwa kwenye Jokofu la kuhifadhia maiti baada ya kuuawa wakati wa majibishano ya risasi na polisi.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC04895
DSC04903
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,akionyesha bunduki ya kijeshi aina ya SMG no.34555  iliyokuwa ikitumiwa na watu wawili wanaodhaniwa kuwa majamabazi katika kijiji cha Manga manispaa ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu).

Msigwa: Baraza la Mawaziri limedumaa

Peter MsigwaMBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), amesema asilimia 40 ya Baraza la Mawaziri limedumaa kwa sababu limeshindwa kutekeleza majukumu yake.

Aliyekuwa DC Mbozi ajiunga CHADEMA

Gabriel Kimollo
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimollo amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Wakazi wa jiji la mbeya wametakiwa kulinda vyanzo vya maji ili kuondokana na tatizo la uhaba wa maji uliopo hivi sasa.

mkurugenzi wa mamlaka ya maji mkoani mbeya Simion  aliongozana na madiwani wa kata ya IGANZO,Mh USWEGE FULIKA na diwani wa kata ya Mwansekwa GASPER NGONELA ambapo wameitaka mamlaka kuzidi kutoa elimu kwa wananchi wanao zunguka vyanzo vya maji.
WADAU WA NISHATI YA UMEME WA MAPOROMOKO YA MAJI NJOMBE WAAHIDI KUFANYA MAKUBWA BAADA YA MAFUNZO.

Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko Madogo ya Umeme Wanaoendelea na Mafunzo Yao ya Wiki Mbili Mjini Njombe Wamesema Tatizo la Fedha Ili Kuendleza Miradi Yao Imekuwa ni Kikwazo Kikubwa Kwao Ili Kusogeza Huduma Kwa Wananchi

Serikali, Tume ya Uchaguzi wavutana



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.PICHA|MAKTABA  
Dar es Salaam. Wakati Serikali ikisema Daftari la Kudumu la Wapigakura litaboreshwa kwa ajili ya kura za maoni ya Katiba Mpya, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema haina mpango huo kwa sababu muda uliobaki ni mfupi.
Badala yake Nec imesema inajiandaa kuboresha daftari hilo kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili kuingiza wale wote waliotimiza miaka 18 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

ANC walaani Zuma kuzomewa, wananchi wadai alistahili hilo


Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.PICHA|MAKTABA  
Johannesburg.Chama Tawala cha Afrika Kusini, Africa National Congress (ANC) kimekasirishwa na kuzomewa kwa Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma wakati wa Ibada ya kitaifa ya heshima za mwisho kwa rais wake wa kwanza mzalendo, Mzee Nelson Mandela.

Ni vilio vitupu A. Kusini



Mjane wa Rais wa Kwanza Mazalendo wa Afrika Kusini, Graca Machel akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe katika Ikulu ya Pretoria nchini humo jana. Picha na AFP  

Pretoria: Familia ya Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela jana iliongoza utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa kiongozi huyo, katika tukio ambalo limebadili mwelekeo wa maombolezo tangu alipofariki dunia, Desemba 5, mwaka huu.

Jeshi la Polisi Singida laua majambazi wawili

WADAU TUNAOMBA RADHI KWA TASWIRA HII KAMA ITAKUKWAZA.
DSC04892
WATU wawili wakazi wa manispaa ya Singida ambao majina yao bado hayajajulikana,wakiwa kwenye Jokofu la kuhifadhia maiti baada ya kuuawa wakati wa majibishano ya risasi na polisi.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC04895
DSC04903
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,akionyesha bunduki ya kijeshi aina ya SMG no.34555  iliyokuwa ikitumiwa na watu wawili wanaodhaniwa kuwa majamabazi katika kijiji cha Manga manispaa ya Singida.(Picha na Nathaniel Limu).

Sunday, 24 November 2013


‘Mtanzania’ akamatwa kesi ya utumwa Uingereza

Polisi wakiwa nje ya moja kati ya majengo yanayohisiwa kutumika kama makazi ya mke na mume waliokamatwa Alhamisi kwa tuhuma za kujihusisha na utumwa. Mmoja kati ya watuhumiwa hao ametokea Tanzania. PICHA | LEON NEAL-AFP 

London. Mmoja kati ya watuhumiwa wawili wanaoshutumiwa kuwashikilia wanawake watatu katika mazingira ya utumwa kwa miaka 30 mjini London anatokea Tanzania, polisi Uingereza wamesema Jumamosi.

Mtei: Tutaendelea kuwafukuza wasaliti


Mwasisi wa Chadema Edwin Mtei anamtaka Saidi Arfi aache kulalamika kwani “kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa mwenyekiti wa Chadema taifa alipaswa kujichunguza kwanza.” PICHA | MAKTABA 

Arusha. Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwafukuza wote wanaokihujumu huku akieleza kwamba, anaunga mkono kuvuliwa uongozi kwa Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.


Laptop ilichangia mauaji ya kutisha Ilala Bungoni

Christina Newa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mauaji yaliyofanywa na mchumba wake Gabriel Munisi. PICHA | MAKTABA 



‘Nilikuwa naomba Mungu kila siku ili afukuzwe Chadema’ - Mama Zitto

 Dar es Salaam. Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.

Thursday, 24 October 2013

  Seif apongeza mkutano wa JK na vyama

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuzungumza na vyama vya siasa kuhusu Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013, akisema ametumia njia sahihi kabisa.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI MKOANI KIGOMA KUZINDUA KIVUKO KIPYA

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI MKOANI KIGOMA KUZINDUA KIVUKO KIPYA CHA MV MALAGALASI WILAYANI UVINZA KESHO.
1_91dbc.jpg
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakati walipokuwa wakimpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo mchana. Makamu amewasili mkoani Kigoma leo kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Malagalasi katika Wilaya ya Uvinza kesho. Picha na OMR

Wednesday, 23 October 2013

Wabunge wastaafu walia njaa kwa Spika

OFISI ya Bunge inaangalia utaratibu wa kufundisha wabunge ujasiriamali baada ya kubainika baadhi ya wanaokoma kushika wadhifa huo, kukabiliwa na hali mbaya ya ukwasi na kulazimika kuomba msaada.

JK: Wakulima ruksa kuuza mahindi nje

Rais Jakaya Kikwete akiwa na wawekezaji wa kampuni ya Sichuan Hongda ya China ambao ni wawekezaji katika eneo lenye utajiri wa chuma la  Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe juzi.

Uswisi sasa kurejesha mabilioni ya mafisadi


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (katikati) akiwa na maafisa wa Serikali ya Uswiss pamoja na timu uchunguzi kufuatilia mabilioni ya fedha zilizowekwa katika benki za nchi hiyo. Picha na Bernhard Reinhold 
Na Fidelis Butahe,Mwananchi

Tuesday, 22 October 2013

Msichana auawa, atumbukizwa chooni

MKAZI wa Kijiji cha Msanzi wilayani Kalambo katika Mkoa wa Rukwa , Festus Sungura (37) anadaiwa kumuua kikatili msichana Janeth Mwanandenje (10) na kisha kutumbukiza mwili wake ndani ya shimo la choo.

Katiba kicheko vyama vyote


Viongozi wa vyama vya Siasa,(kushoto)Isaack Cheyo(UDP) Nancy Mrikaria(TLP) Fahmi Nassoro Dovutwa (UPDP),James Mbatia NCCR-Mageuzi,Profesa Ibrahim Lipumba(CUF),Philip Mangula(CCM) na Dk Willibrod Slaa(Chadema)wakiwa wameshikana mikono baada ya kikao cha pamoja jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix 

Sunday, 20 October 2013

Boko Haram waua madereva 19 Nigeria

131015124213_nigeria_bokoharam_304x171_afp_acd2c.jpg
Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.
130920090824_nigeria_304x171_ap_13bd5.jpg
Mabaki ya magari ya madereva waliouawa na Boko Haram
Wanaume hao waliokuwa wamejihami , waliwasimamisha madereva na kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari yao kabla ya kuwapiga risasi na kuwaua.
Walioshuhudia tukio hilo waliambia BBC kuwa wanaume hao walikuwa wanachama wa Boko Haram, ingawa kundi hilo bado halijatamka chochote kuhusu mauaji hayo.
Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na serikali kutaka utawala wa kiisilamu.(P.T)
Kundi hilo huwalenga raia na wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na jeshi la taifa.
Shambulizi la hivi karibuni, lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji wa Logumani, ambao hauko mbali sana na mpaka na Cameroon.
Walionusurika shambulizi hilo walisema kuwa washambuliaji walivaa nguo za jeshi na walikuwa wanaendesha pikipiki kabla ya kuwashambulia waathiriwa.
"Takriban wanaume 9 walituamuru kuondoka kwenye magari yeu na kulala chini,'' alisema mwanamume
"Waliwaua watu 5 kwa kuwapiga risasi na kasha kuwanyonga wengine 14 kabla ya mtu mmoja kuwapigia simu na kuwambia kuwa wanjeshi wanakuja.''
Alisema washambuliaji baadaye walitoroka na kujificha msituni kwa pikipiki zao.
Manusura mwingine alisema kuwa alisikia mtu aliyekuwa karibu naye akiuawa kwa kisu. Alisema ana uhakika kuwa washambuliaji walikuwa Boko Haram kwa sababu ya kuwa na ndevu.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alisema kuwa ni jambo la kawida kwa polisi kuweka vizuizi barabarani hasa katika maeneo yenye misukosuko na huenda washambuliaji waliiga mbinu hioyo ya jeshi ili kuwanasa waathiriwa. I,
Boko Haram limezua mgogoro mkubwa wa kisiasa Nigeria tangu mwaka 2009, nia yao kuu ikiwa kuunda utawala wa kiisilamu, hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi
Kundi hilo limelaumiwa kwa mashambulizi kadhaa ambao yamesababisha takribna vifo 2,000 tangu mwka 2011.

... Kufumba Na Kufumbua Simba Wamesawazisha...!

1004981_10201511310877418_1416046447_n_536ae.jpg
Ama kweli, kutangulia si kufika, na hasa kama unatumia baiskeli kama ya ' Mwenyekiti'...!
Maggid.
Iringa.(P.T)

Askari wa Hifadhi waingia kashfa nyingine ya mauaji

6_29584.jpg
NA DANIEL LIMBE
Askari wa Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo wilayani Geita mkoani hapa, wamekumbwa na kashfa nyingine baada ya kudaiwa kumuua raia mmoja kwa kipigo mbele ya kituo kidogo cha polisi Chato.

Utafiti wabashiri Katiba mpya

WAKATI Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiandaa rasimu ya pili ya Katiba itakayopelekwa katika Bunge la Katiba, utafiti uliofanywa na asasi ya kimataifa umebashiri baadhi ya matokeo ya Katiba ijayo.

Wednesday, 16 October 2013

Samaki wabovu waielemea Serikali

 
Msemaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Roida Andusamile amekiri kuwa shirika hilo lilikutana na samaki hao kabla hawajaletwa nchini. PICHA|MAKTABA 

Tuesday, 15 October 2013

Mama yake Ufoo alipigwa risasi tano


TAARIFA zaidi za kusikitisha kuhusu mauaji ya kinyama, yaliyofanyika katika familia ya Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro zimeendelea kutolewa, ambapo imebainika mama mzazi wa mtangazaji huyo, Anastazia Saro (58), aliuawa kwa kupigwa risasi tano.

GARI LA MWISHO KUTUMIWA NA MAREHEMU BABA WA TAIFA,NA MAGARI MENGINE YA SERIKALI ALIYOKUWA AKIYATUMIA ENZI ZA UHAI WAKE

Mwalimu kambarage
Hili ni gari ambalo marehemu baba wa Taifa ambae leo anatimiza miaka 14 tangu kufariki kwake alilitumia wakati anapelekwa Airport kwaajili ya matibabu.

Hali ya muandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro inaendelea vizuri.

Hali ya muandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro aliyejaruhiwa kwa risasi na mzazi mwenzie inaendelea vizuri lakini bado yupo chini ya uangalizi maalum wa madaktari.

Kwa mujibu wa madaktari waliomfanyia upasuaji wa kuondosha risasi iliyokuwa tumboni Ufoo anahitaji muda mwingi wa kupumzika ili aweze kupata nafuu na kurudi katika hali yake ya kawaidia.



Muandishi huyo alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Tumbi Kibaha Mkoani Pwani ambapo alipelekwa mara baada ya kukutwa na tukio hilo.

Wednesday, 9 October 2013

Wawekezaji wanyanyasaji kufukuzwa


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema wawekezaji watakaobainika kujishughulisha na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia pamoja na kuwasumbua wafanyakazi katika sekta za mahoteli watachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa nchini.

Mfanyabiashara Arusha adai kumwagiwa tindikali


MFANYABIASHARA Japhet Minja amelazwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Centre (Seliani) jijini Arusha, baada ya kumwagiwa kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali usoni na watu wasiojulikana.

Vurugu mgomo wa mabasi na malori

MGOMO wa malori na mabasi kupinga Sheria ya Barabara inayowataka wasiongeze mizigo kupita kiwango cha mwisho cha uzito, umeingia katika sura nyingine ambapo baadhi ya wasemaji wa wamiliki, wamewasingizia viongozi kuwa wamelegeza msimamo.

Mazishi ya kitaifa kwa wahamiaji Lampedusa

zzzzlampedusa_cuerpos_italia_304x171_reuters_nocredit_a7059.jpg
Serikali ya Utaliana itafanya mazishi ya kitaifa kwa mamia ya wahamiaji waliokufa maji baada ya boti walimokuwa wanasafiria kuzama katika bahari ya Meditarenia kisiwani Lampedusa wiki iliyopita.

Marubani wageni ‘wavamia’ soko la ajira Tanzania

MarubaniClip 0a0b9
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesema ajira ya marubani wazalendo ipo mashakani kwa sababu ndege nyingi nchini, zinaongozwa na wageni.TCAA imesema hali hiyo imekuwa ikichangiwa na kampuni zinazotoa huduma hizo nchini, kutumia ndege nyingi za kukodi zinazofanya kazi chini ya masharti yanayotoa nafasi kubwa ya kuongozwa na marubani wa kigeni.(hd)

USALAMA ‘FEKI’ ANASWA MTEGONI



IMG 4926 e7e26

MULUGO ATAKA WALIOKOSA MIKOPO KUJISOMESHA

148 Philipo-Mulugo1 57d1b
Na Gladness Theonest
Serikali imewataka wanafunzi waliokosa mikopo kwa ajili ya masomo vyuo vikuu kurudi nyumbani na ikiwezekana wakauze viwanja au ng'ombe ili waweze kujisomesha kwani bajeti iliyopo haitoshi.

sakata la kodi ya simu

Fatma Karume 75d49
Wanasheria Fatma Karume (kulia) na Beatus Malima wanaowakilisha Chama cha Walaji nchini wakijadiliana na mawakili wa Serikali, Alesia Mbuya (wa pili kushoto) baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuahirisha kesi ya kupinga kukatwa kodi ya Sh, 1,000 kwa kila simcard ambayo ilipitishwa na Bunge la Bajeti la mwaka huu wa fedha wa 2013/149 (hd)

Monday, 7 October 2013

Tundu Lissu amjibu JK

siku-tundu-lisu-alipokutana-na-jk-ikulu-jijini-dar-es-salaam_f685e.jpg
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu amesema hotuba ya kila mwezi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa siku tatu zilizopita, imejaa maneno mengi ya kuambiwa hasa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, ikiwa ni pamoja na uteuzi alioufanya wa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Mbunge ajitoa ujumbe bodi ya CDA kupinga bomoabomoa

 mji fa4dc
NA JACQUELINE MASSANO
Mbunge wa Dodoma Mjini, David Malolle (CCM), ametangaza rasmi kujitoa kwenye ujumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na kuwataka wananchi kuandamana ili mamlaka hiyo ifutwe kwani imekuwa ikibomoa mji na si kuuboresha.(hd)

Kauli ya serikali Juu ya mgomo wa Wasafirishaji


Picha_1_1fb96.jpg
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisisitiza jambo kuhusu mgomo uliopangwa kufanywa na wadau wa usafirishaji nchini wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar Es Salaam

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAshinda VIKOMBE VITATU NA MEDALI TATU-SHIMI​WI DODOMA

PIX 1 ede04

Wednesday, 2 October 2013

VURUGU KUBWA ZIMEZUKA TENA WAKATI WAFANYABIASHARA WAKISUBILI MKUTANO WAKATI HUU ENDELEA KUFUATILIA MTANDAO HUU KWA TAARIFA ZAIDI.

Wafanya Biashara wakiwa wanajiandaa kusikiliza mkutano muda mchache uliopita na Ghafla vurugu kuzuka tena ....

MBEYA KIMENUKA.

 Polisi wakiwa katika ulinzi mkali 
 Maduka yakiwa yamefungwa 
 Wafanya biashara wakiwa uwanjani kungoja kusikiliza nini  hatma yao
 Baadhi ya watu wakiwa wanakimbia Baada ya Mabomu ya machozi kuanza kurushwa kuepusha vurugu
 Mawe yakiwa yamepangwa kuzuia magari yasiende kokote
 Maduka yote yakiwa yamefungwa eneo la mwanjelwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA
 Vijana hawa wakiwa wana nawa uso baada ya Bomu la machozi kuwapitia 
 Jiwe kubwa likiwa limewekwa katika Barabara magari yasipite
 Hali tete Tayari vijana wameanza kuchoma mataili.....