Pages

Tuesday, 20 August 2013


NJOMBE
Jamii wilayani Ludewa mkoani Njombe, imetakiwa kutoa ushirikiano katika kipindi hiki cha ujenzi wa barabara unaoendelea kuanzia Ludewa maeneo ya Kilimahewa mjini Ludewa hadi kijiji cha Lupingu.
Na Festus Pangan
endelea....
Akizungumza na Radio Best Fm hii leo, Meneja wa tanroads mkoani njombe injinia Mazanda Yusuph amesema mradi huo ambao unajengwa na kampuni ya ukandarasi ya Boimanda Morden Contractors inatarajiwa kukamilika kabla ya kipindi cha masika.
Injinia mazana amebainisha kuwa pamoja na ushirikiano ambao umekuwa ukitolewa na jamii wilayani ludewa, barabara hiyo inatarajiwa kufungua njia za mawasiliano kwa wananchi wilayani humo ikiwemo kusafirisha mazao yao ili kujiletea maendeleo.
Kwa mujibu wa  taarifa ya  kikao cha bodi ya barabara mkoa wa njombe ambacho kiliketi mwezi wa saba mwaka huu, kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara kwa mwaka wa fedha 2012|2013 kazi zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na kuondoa maporomoko ya udongo kusafisha mifereji kuanzia Ludewa hadi kijiji cha Lupingu.
Kazi nyingine zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na kukata ili kupanua barabara, kuondoa maporomoko ya udongo, kuchonga barabara, kuondoa mawe, pamoja na kuchimba mifereji nje ya barabara ambapo hadi sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 100.

TAARIFA YA POLISI.
NJOMBE.
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti mkoani njombe likiwemo la Mtoto mmoja VAILETH SAMBALA mwenye umri wa miezi 7, mkazi wa Lupanga wilayani ludewa mkoani njombe amefariki dunia baaba ya kutumbukia kwenye ndoo yenye maji.
Katika tukio la kwanza kamanda wa polisi mkoa wa njombe FULGENCI NGONYANI amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane kamili mchana katika kijiji cha Lupanga kata ya Lupanga wilayani Ludewa.

No comments: