Pages

Thursday, 15 August 2013

MANISPAA YA IRINGA YAMALIZA UTATA KATI YA MACHINGA NA POLISI ENEO LA MASHINE TATU YAGEUZA STENDI YA DALADALA

 Daladala  zikiwa  zikisubiri abiria  katika  stendi mpya  ya Mashine  tatu  katika Manispaa ya Iringa eneo  ambalo awali  machinga  walikuwa  wakilitaka kwa shughuli zao  siku za  jumapili
Na Meck Lameck
 
endelea.....
 Hili  ndilo  eneo maarufu  la  kihistoria katika  mji  wa Iringa  eneo la Mashine  tatu
Daladala  zikiwa katika  stendi  mpya  ya soko la Mashine  tatu na chini ni  picha  za maktaba  yetu  jinsi  hali  ilivyokuwa awali

mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akiwasili eneo la vurugu kabla ya kuanza kwa vurugu hizo
Mbunge Msigwa akiondoka eneo la mashine tatu
Machinga wakisukuma gari ya mbunge Msigwa
Polisi wakimfuatilia mbunge Msigwa kwa nyuma baada ya kufika eneo hilo bila kufanya biashara kama alivyoahidi
Hali ikiendelea kuwa tete kwa machinga kufunga barabara kuu ya Iringa Dodoma na ile ya mashine tatu

Ni Machafuko Iringa
HALMASHAURI ya  Manispaa ya  Iringa  mkoani Iringa  imefanikiwa kumaliza  utata  uliokuwepo kati ya  wafanyabiashara  ndogo  ndogo (Machinga) na  polisi baada ya  kuligeuza  eneo  lililokuwa  likigombewa na machinga  eneo la mashine  tatu  kuwa stendi  ya  daladala zinazofanya  safari  zake nje ya mji  wa Iringa .

Mtandao  huu  wa  matukiodaima.com umetembelea  eneo hilo na  kushuhudia  eneo  hilo  likiwa  tulivu  kwa  sasa  baada ya  kugeuzwa  kuwa  eneo la  stendi ya daladala .
Wakizungumzia  hatua  hiyo ya  uongozi  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  kugeuza  eneo  hilo kuwa  stendi ya  daladala Bw  Omari All na Kevin Sanga  ambao ni  machinga mjini Iringa  mbali ya  kupongeza hatua  hiyo  ambayo  wamedai  imeipusha machafuko  zaidi ila  bado  wameomba  uongozi wa Manispaa ya  Iringa  kuwaboreshea  eneo la Mlandege  ambalo wanaendelea  kulitumia kwa  shughuli za gulio kila jumapili.
Kwa  walisema  kuwa  eneo hilo la mashine  tatu ambalo  sasa limefanywa stendi ya  daladala  lilikuwa  ni  zuri  zaidi  kwao kiuchumi  ila kwa  kuwa  serikali  iliwataka  kuondoka eneo hilo hawanapingamizi  na uamuzi  huo wenye  sura ya kuuweka mji katika mpangilio mzuri zaidi.
"Sisi  hatuna  pingamizi  lolote  na  uamuzi wa Manispaa kugeuza  eneo hili  stendi ya  daladala ila  bado tunaomba  kuboreshewa mazingira  ya gulio la Mlandege ama  kupewa  eneo la barabara  mbili kwa  siku  za  jumapili"
Huku  Madereva  wa  daladala  katika  stendi hiyo wakidai  kuwa  eneo hilo  awali  ilikuwa ni gumu kujulikana kwa abiria  ila kwa  sasa wananchi  wengi  wamelitambua hivyo hakuna tatizo  lolote kwao.

No comments:

Post a Comment