Hali ya muandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro inaendelea vizuri.
Hali
ya muandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro aliyejaruhiwa kwa
risasi na mzazi mwenzie inaendelea vizuri lakini bado yupo chini ya uangalizi
maalum wa madaktari.
Kwa
mujibu wa madaktari waliomfanyia upasuaji wa kuondosha risasi iliyokuwa tumboni
Ufoo anahitaji muda mwingi wa kupumzika ili aweze kupata nafuu na kurudi katika
hali yake ya kawaidia.
Muandishi
huyo alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Tumbi
Kibaha Mkoani Pwani ambapo alipelekwa mara baada ya kukutwa na tukio hilo.
Ufoo
alipigwa risasi ya mguuni na tumboni na mzazi mwenziwe maeneo ya Kibamba CCM
nyumbani kwa mama yake Anastazia Peter Saro ambaye naye aliuwawa kwa kupigwa
risasi na Ansel Mushi mzazi mwenzie na muandishi huyo.
Kwa mujibu wa Kamishna wa polisi Kanda maalum
ya Dar es Salaam Suleiman Kova dalili za tukio hilo zinaonyesha kuwa ni
masuala ya kifamilia na uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini chanzo chake.

No comments:
Post a Comment