Pages

Thursday, 12 December 2013

WADAU WA NISHATI YA UMEME WA MAPOROMOKO YA MAJI NJOMBE WAAHIDI KUFANYA MAKUBWA BAADA YA MAFUNZO.

Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko Madogo ya Umeme Wanaoendelea na Mafunzo Yao ya Wiki Mbili Mjini Njombe Wamesema Tatizo la Fedha Ili Kuendleza Miradi Yao Imekuwa ni Kikwazo Kikubwa Kwao Ili Kusogeza Huduma Kwa Wananchi


Wakizungumza na mecklameck blogspot.com Mara baada ya Kufanya Ziara ya Kwenda Kutembelea Vyanzo Vya Umeme wa Maporomoko ya Maji vya Mawengi na Chanzo cha Mkongobati Wilayani Ludewa Jana wadau hao wamesema kuwa kutokana na hali ya miradi yao imekuwa ikienda kwa kusuasua kutokana na kukosa namna ya kuomba ufadhili toka
maeneo tofauti.

Pamoja na mambo mengine wameeleza kuwa ili kurahisisha tatizo hilo wanatarajia Kuunda umoja wao utakaorahisisha upatikanaji wa fedha toka serikali kupitia vikundi vyao.

Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo katika kundi la pili litakalohitimu disemba 17 mwaka huu Mhandisi Emmanuel  Michael amesema kuwa kutokana na elimu aliyoitoa kwa siku zote pamoja na mafunzo ya vitendo itawafanya wadau hao kupanua wigo wa kuongeza miradi hiyo pamoja na kuomba ufadhili toka kwa wahisani mbalimbali.

Mhandisi Emmanuel Amesema Miongoni mwa mambo Aliyofundisha ni pamoja na kujua namna ya kuandika maandiko mbalimbali ya kuomba ufadhili na mbinu za kuomba mikopo kwenye taasisi nyingine za kifedha kwani wengi wao hawakufahamu watapata wapi wafadhili

Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme wa maporomoko ya maji kutoka katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini Chini ya ufadhili wa Wakala wa nishati Vijijini REA watakao hitimu Disemba 15 na 17 mwaka huu.

No comments: