POLISI 7 'FEKI' MBARONI DAR
- WALIVALIA SARE,MMOJA ANA CHEO CHA MEJA
- YADAIWA WALIKUWA 'DORIA' MAENEO YA BOKO
- OFISA USALAMA BANDIA NAYE ABAMBWAENDELEA....
SIKU chache baada ya trafiki feki mwenye
cheo cha sajini kukamatwa jijini Dar es Salaam akiongoza magari, mapya yamezidi
kuibuka baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam kufanikiwa kuwakamata watu saba wanaotuhumiwa kuwa majambazi
wakiwa wamevalia sare za jeshi hilo
wakiwa na vyeo tofauti.
Mbali
watu hao, Polisi pia amemkata mkazi mwingine wa jijini Dar
es Salaam akijifanya Ofisa wa Usalama wa Taifa, huku akiwa na
nyaraka mbalimbali za Serikali kutoka Ofisi za Uhamiaji na kitambulisho chake
cha kazi, ambacho alikuwa akikitumia kabla ya kustaafu Jeshi la Ulinzi la
Wananchi wa Tanzania
(JWTZ). Pia alikamatwa na bastola mbili zikiwa na risasi 12 na baada ya
kufanyiwa upekuzi nyumbani kwake alibainika kumiliki bastola nyingine ya tatu
ikiwa na risasi 19.
Kukamatwa kwa watu hao kulithibitishwa na Kamishna wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Sulemain Kova, alipozungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana.Alisema katika
tukio la kwanza Polisi walifanikiwa kukamata watu saba wanaodaiwa kuwa
majambazi wakiwa wamevalia sare hizo, huku mmoja akiwa na cheo cha Meja ambapo
sare yake ilionesha beji inayosomeka SSGT A.M Mduvike.
Alisema
watuhumiwa wengine wengine walikuwa Jeshi la Polisi linamshikilia Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Ramadhan Semsota (63)
kwa kosa la kujeruhi kwa risasi fundi ujenzi, Fadhili Mkachino. Tukio hilo lilitokea maeneo ya
Salasala jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment