NJOMBE
Jamii wilayani Ludewa mkoani Njombe, imetakiwa kutoa
ushirikiano katika kipindi hiki cha ujenzi wa barabara unaoendelea kuanzia
Ludewa maeneo ya Kilimahewa mjini Ludewa hadi kijiji cha Lupingu.
Na Festus Pangan
Akizungumza na Radio Best Fm hii leo, Meneja wa tanroads
mkoani njombe injinia Mazanda Yusuph amesema mradi huo ambao unajengwa na
kampuni ya ukandarasi ya Boimanda Morden Contractors inatarajiwa kukamilika
kabla ya kipindi cha masika.
Injinia mazana amebainisha kuwa pamoja na ushirikiano ambao
umekuwa ukitolewa na jamii wilayani ludewa, barabara hiyo inatarajiwa kufungua
njia za mawasiliano kwa wananchi wilayani humo ikiwemo kusafirisha mazao yao
ili kujiletea maendeleo.
Kwa mujibu wa taarifa
ya kikao cha bodi ya barabara mkoa wa
njombe ambacho kiliketi mwezi wa saba mwaka huu, kwa ajili ya matengenezo na
ukarabati wa barabara kwa mwaka wa fedha 2012|2013 kazi zinazotarajiwa
kutekelezwa ni pamoja na kuondoa maporomoko ya udongo kusafisha mifereji
kuanzia Ludewa hadi kijiji cha Lupingu.
Kazi nyingine zinazotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na kukata
ili kupanua barabara, kuondoa maporomoko ya udongo, kuchonga barabara, kuondoa
mawe, pamoja na kuchimba mifereji nje ya barabara ambapo hadi sasa utekelezaji
wake umefikia asilimia 100.
TAARIFA YA POLISI.
NJOMBE.
Watu wawili wamefariki dunia katika matukio mawili tofauti
mkoani njombe likiwemo la Mtoto mmoja VAILETH SAMBALA mwenye umri wa miezi 7, mkazi
wa Lupanga wilayani ludewa mkoani njombe amefariki dunia baaba ya kutumbukia
kwenye ndoo yenye maji.
Katika tukio la kwanza kamanda wa polisi mkoa wa njombe
FULGENCI NGONYANI amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa nane kamili
mchana katika kijiji cha Lupanga kata ya Lupanga wilayani Ludewa.
No comments:
Post a Comment