38 wafa kwa mafuriko Sudan
KHARTOUM, Sudan
WATU wasiopungua 38 wanaripotiwa kupoteza maisha nchini Sudan baada ya kutokea mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko.
endelea
Watu hao wamekufa kutokana na matukio mbalimbali yaliyosababishwa na mafuriko yakiwemo kubomoka nyumba zao, kusombwa na maji au kupigwa na shoti ya umeme. Aidha janga limesababisha maelfu ya nyumba kubomoka na hivyo kuwaacha bila makazi watu wengi wa maeneo ya kaskazini katika Jimbo la Darfur. Maelfu ya familia katika maeneo ya mashariki zinakabiliwa na hali mbaya huku nyumba zao zikiwa zimesombwa na mafuriko hayo.
Tayari Serikali ya Sudan imeanza kupeleka misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo.
No comments:
Post a Comment