KONDA WA DALADALA IRINGA AFANYISHWA USAFI BAADA YA KUNASWA AKIJISAIDIA HADHARANI
Kijana anayefanya kazi ya ukonda
katika daladala inayofanya safari zake kati ya Kitapilimwa - M.R
miyomboni Bw Christipher Kinigo akifanya usafi wa kuzoa taka kwa
mikono baada ya kunaswa akijisaidia haja ndogo katika eneo hilo
kinyume na sheria za usafi Manispaa ya Iringa
Na Meck Lameck
endelea....
Hapa akitafakari jinsi ya kuzoa
taka kwa mikono baada ya kushindwa kulipa faini ya Tsh 50,000
iliyopangwa na Manispaa ya Iringa kwa wachafuzi wa mazingira
Hapa akiwajibika kufanya usafi
Hapa koda huyo Bw Christopher
anayefanyia kazi katika daladala lenye namba T 228 AMV akizoa taka
katika dampo la M.R mchana wa leo
Konda huyo akiwa katika daladala analofanyia kazi baada ya kufanya usafi kama adhabu ya kuchafua mazingira.
KONDA wa daladala lenye namba T 228 AMV
inayofanya safari zake kati ya Kitapilimwa na M.R- Miyomboni mjini
Iringa Bw Christopher Kinigo amepewa adhabu ya kuzoa taka katika
dampo kwa mikono baada ya kukutwa akijisaidia haja ndogo kituo cha
daladala M.R kando ya barabara ya Mkwawa .
Kijana huyo amekamatwa leo na wadau
wa mazingira mjini Iringa ambao wamekuwa wakifanya kazi na mtandao
wa matukio daima katika kuweka mji wa Iringa na mkoa wa Iringa katika
hali ya usafi.
Hatua ya kijana huyo kufanyishwa
usafi imekuja baada ya kuangua kilio akiomba kusamehewa kutokana na
kosa hilo na kuwa hakuwa na fedha kiasi cha Tsh 50,000 ambazo ni
faini za kisheria kwa wanaokamatwa kwa kuchafua mazingira katika
mji wa Iringa.
Akizungumza baada ya kutekeleza zoezi
hilo la usafi kijana huyo alisema kuwa ugeni ndio ambao unamsumbua
na kuwa anatambua kosa lake na kuwataka vijana wenzake na
wananchi wengine kuepuka kuchafua mazingira katika mji wa Iringa.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa Manispaa
ya Iringa Innocent Kihanga mwananchi atakayekutwa anachafua mazingira
kwa kutupa taka ovyo ama kujisaidia maeneo yasiyo rasmi faini yake
Tsh 50,000 na mkamataji atalipwa Tsh 20,000 na fedha nyingine
zitaingizwa katika mfuko wa usafi wa mazingira mjini Iringa.
Hivyo kuwataka wananchi kuendelea
kuwakamata na kuwafikisha ofisi ya manispaa ya Iringa wale wote
wanaochafua mazingira ovyo .
Huku mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo akipongeza jitihada za wadau wa
mazingira mjini Iringa na kutaka kila mwananchi kuhakikisha eneo
lake ni safi .
No comments:
Post a Comment