KERO YA MAJI YAWATESA WANANCHI WA KIJIJI CHA NJELENJE MBEYA
Na Esther Macha,wa matukiodaima.com mbeya
WANANCHI wa Kata ya Mshewe kijiji cha Njelenje Wilaya ya Mbeya
wamelalamikia kutokuwa na maji kwa muda
wa miaka 10 licha ya uongozi wa kata
hiyo kuendelea kuwachangisha michango ya
mabomba wananchi hao .
Na Meck
Wamesema ni jambo la kusikitisha kuona uongozi uliopo kufanya kazi ya kuchangisha michango
tangu mwaka 2009 mpaka sasa na dalili za
kuwepo maji hakuna na hata kusomewa mapato na matumizi ya fedha hizo hayapo.
Uchunguzi uliofanywa na Mtandao huu kwa kushirikiana na
Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) umebaini kuwa maji ambayo wanatumia wananchi
wa kijiji hicho ni yale ambayo yanatoka kwenye chanzo ambacho ni makaburi ya
watu ambayo hata hivvyo hayana usalama wowote.
Hata hivyo majira
ilibaini kuwa maji hayo ambayo yapo kwen ye chem chem. Makaburi makazi yua watu ambako kuna vyoo kwa ujumla
yanahatarisha afya za wananchi wa eneo
hilo hususan watoto wadogo.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Njelenje Bw.Rashid Odati alisema kuwa
toka wameanza kuchangia maji ni muda mrefu, kwani maji yaliyopo ambayo
wanatumia ni hatari kwa afya za wananchi
kutokana na maji wanayotumia kutoka kwenye
chanzo ambacho kipo karibu na vyoo na makaburi ya watu.
“Hapa tulipo hatuelewi hatima yetu ni nini kwani maji
tunayotumnia ni hatari sana kwa afya zetu hebu ndugu mwandishi wa habari
angalia hicho chanzo kipo kati kati ya makaburi
kwa hali hii sidhani kama kuna uhakika wa sisi wananchi kupata maradhi”alisema
Mkazi huyo.
Akizungumzia kuhusu viongozi alisema wamekuwa na sababu
nyingi za kutoa kwa wananchi ambazo hazina umuhimu wowote kutoka kwa wananchi
kwani fedha ambazop zinachangwa na
zimekuwa kama mtaji kwao wa kuendeshea maisha yao.
“Mfano huyu diwani wetu
amekuwa na amri zake kwa wananchi
kwa kutumia cheo chake
kukandamiza wananchi ,sisi hatutaki diwani awe mwiba kwetu kwa
kutumia nafasi yake kama fimbo kwa wananchi “alisema Bw. Odati.
Mkazi mwingine Bi.Teddy Mwakaje alisema kutokana na shida ya
maji hakuna maendeleo yeyote ambayo wanafanya kutokana na muda mwingi kutumia
kutafuta maji kwani hata yaliyopo kwenye
chazo nayoi bado ni tatizo kuyapata licha ya kutokuwa na usalama wa kutosha.
Akizungumzia tatizo hilo la maji Mwenyekiti wa kitongoji cha
Kizota Bw. John Kapange alisema kuwa kero hiyo ya
maji ni ya muda mrefu katika kijiji
hicho na kusababisha wananchi kutoka usiku wa manane kwenda kutafuta
maji kwenye visima.
Akijibu malalamiko hayo ya wananchi Diwani wa
Kata ya Mshewe Bw.Fabian
Mwakasole alisema tatizo hilo la
maji katika kijiji cha Njelenje ni la
muda mrefu na kwamba toka anaingia madarakani mwaka 2010 amelikuta.
No comments:
Post a Comment