Pages

Saturday, 28 September 2013

Viongozo wa Dini wawaonya viongozi siasa;

viongoziwa_dini_4b67f.png
VIONGOZI wa dini waonya baadhi wanasiasa mbele ya waziri wa Afrika mashariki Bw Samweli Sitta kuwa vita na vurugu nchini zinasababishwa na wanasiasa wenye uchu wa kutaka kuingia Ikulu mwaka 2015.

Akizungumza katika makaburi ya Mlolo mjini Iringa jana wakati wa mazishi ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Urambo marehemu Anna Magoha ,kiongozi wa Dhinuren Iringa Abdulsalaam Ayub ,alisema kuwa si kweli kama wakristo na waislam nchini na maadui kiasi cha kuanza kupigana na kuuwawa ila vurugu zinazotokea nchini zinasababishwa na wanasiasa ambao wanatumia mbinu hiyo chafu kutaka kuingia Ikulu .(P.T)

Kwani alisema hali ya amani ya Tanzania si mbaya kama ilivyo katika nchi nyingine ambazo tumekuwa tukisikia ama kushuhudia katika vyombo vya habari machafuko yanayoendelea .
" Si kweli kama baadhi ya wanasiasa wanavyosema kuwa dini ndivyo zinachochea vurugu hapa nchini kwani waislam hawaweze kukusanya watu kwa ajili ya kuvuruga amani kwani hata dini hiyo hairuhusu "
Ayub alisema wakristo na waislam siku zote wamekuwa ni marafiki na haijapata kutokea machafuko ila sasa hivi baadhi ya viongozi wa siasa wanawagombanisha kwa maslahi yao ya kisiasa.
" Ninasema kuwa baadhi ya wanasiasa ndio wanaogombanisha wakristo na waslamu na natamka wazi kuwa sitaweza kufuta kauli hii hadi ninapo kufa kwani huo ndio ukweli wenyewe .....watu wanalitamani lile jingo jeupe jirani na bahari pale na ndio wanaotuchafulia amani yetu"
Kwa upande wake waziri Sitta alisema kuwa umoja na amani haiwezi kupatikana kama watanzania hatutakuwa wamoja na kuwa amani ya Taifa letu inatazamwa kwa jicho baya na nchi zisizopenda amani.
Waziri Sitta alisema kuwa Tanzania ni nchi ambayo ina amani kubwa na kuwa hata yule ambae atataka kuvuruga amani yetu ni lazima kufanya kazi kubwa kwani Rais Jakaya Kikwete amefanya kazi kubwa katika kuimarisha amani na kila mtanzania anapaswa kuendeleza amani iliyopo.
Hata hivyo alivitaka vyama vyote vya siasa kuendelea kuheshimu amani iliyopo na kuwa vyama vyetu vya siasa na nafasi za uongozi zisisababishe Taifa kukosa amani.
Akielezea juu ya kifo cha mkuu huyo wa wilaya ya Urambo alisema kuwa wilaya hiyo na mkoa wa Tabora umepata pigo kubwa kwa kifo hicho kwani mkuu huyo ndie aliyepigania ujenzi wa shule za sekondari na ujenzi wa barabara za lami na katika kumuenzi baadhi ya shule na barabara zitapewa jina lake la Anna Magoha kama sehemu ya kutambua mchango wake.

No comments: