39 wauawa madukani Kenya, Al-Shabab yakiri kuhusika
Polisi wa Kenya akimuokoa mtoto, baada ya kundi la watu waliokuwa na
silaha kuvamia duka kubwa la bidhaa katika jengo la Wastgate, jijini
Nairobi, jana na kuwaua zaidi ya 20 na wengine kuwajeruhi.
Kwa ufupi
- Tukio hilo lilitokea jana mchana ambapo watu waliokuwa wakizungumza lugha ya kigeni, inayodhaniwa kati ya Kiarabu au Kisomali, kuvamia jengo la ghorofa na kushambulia watu kwa risasi.
Nairobi. Zaidi ya watu 39
wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuliteka
jengo lenye maduka la Westgate, jijini Nairobi, Kenya.
Tukio hilo lilitokea jana mchana ambapo watu
waliokuwa wakizungumza lugha ya kigeni, inayodhaniwa kati ya Kiarabu au
Kisomali, kuvamia jengo la ghorofa na kushambulia watu kwa risasi.
“Hawakuwa wakizungumza Kiswahili. Walikuwa
wakizungumza kwa lugha kama vile Kiarabu au Kisomali, lakini sina hakika
sifahamu lugha hizo,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyefanikiwa kutoka
ndani ya jengo hilo na kujitambulisha kwa jina moja la Jay.
Shuhuda mwingine aliyejitambulisha ni mfanyakazi
wa Ubalozi wa Uholanzi jijini Nairobi, Rob Vandijk, alisema tukio hilo
lilitokea wakati akipata chakula cha mchana ndani ya njengo hilo.
Alisema watu hao waliingia ndani ya jengo la maduka hayo na kuanza kushambulia watu kwa risasi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Abbas Guled alisema: “Ninachoweza kusema tuna takriban maiti 20. Majeruhi ni wengi.”
Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja baadaye,
Rais Uhuru Kenyatta alithibitisha kuwa zaidi ya watu 39 walikufa katika
shambulizi hilo la kinyama, na wengine 150 kujeruhiwa.
"Vyombo vya usalama vinafanya kila jitihada
kuthibiti eneo hili na kuwakamata waliohusika," asema Mr Kenyatta,
akiongeza kuwa naye pia amepoteza wanafamilia katika tukio hilo.
Polisi Waingia
Taarifa zingine zilisema kuwa polisi waliwasili eneo la tukio dakika 30 baada ya watu hao kuvamia jengo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kenya, Inspekta Jenerali
David Kimaiyo alisema kwamba polisi walifika katika jengo hilo baada ya
kupata taarifa, ambapo nao walianza kujibizana kwa risasi na magaidi hao
waliokuwa hapo ndani.
Alisema watu hao wanaosadikiwa ni magaidi walikuwa
wakijaribu kuiba pesa katika jengo hilo, kabla ya polisi hawajatokea na
kuanza kurushiana risasi.
No comments:
Post a Comment