Rais Kikwete aongoza mazishi ya Askofu Kulola
Waziri Mkuu aliyejiuzulu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa jana wakati wa
ibada ya mazishi ya Askofu Mkuu, Moses Kulola wa Kanisa la Evangelist
Assemblies of God Tanzania (EAGT) aliyezikwa nje ya Kanisa la Calvary
endelea......
Kwa ufupi
- Alikuwa askofu wa ajabu sana, hata kama ungeweza kumtandikia mkeka ili alale, angelala. Jambo hili ni tofauti sana na maaskofu wa kileo ambao ukiwatendea hivyo watanung’unika na kukusema kila siku.
Mwanza.
Rais Jakaya Kikwete ameongoza maelfu ya waombolezaji kumzika aliyekuwa Askofu Mkuu Moses Kulola wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT). Kiongozi huyo alizikwa jana nje ya Kanisa la Calvary Bugando.
Rais Jakaya Kikwete ameongoza maelfu ya waombolezaji kumzika aliyekuwa Askofu Mkuu Moses Kulola wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT). Kiongozi huyo alizikwa jana nje ya Kanisa la Calvary Bugando.
Licha ya kuongoza mazishi hayo, Rais Kikwete pia
alitoa ushuhuda kwamba licha ya kuwa muumini wa dini ya Kiislamu, Askofu
Kulola wakati wa uhai wake mara kadhaa alikwenda Ikulu kumfanyia
maombi.
Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi,
alisema amekwenda kushiriki msiba huo kuungana na waombolezaji kutokana
na kumfahamu Askofu Kulola ambaye alikuwa mtu wa watu.
“Tuzidi kuwaombea kwa Mungu, familia katika
kipindi hiki kigumu, kwa jinsi nilivyomfahamu marehemu alikuwa mpenda
watu, hakujali kabila wala hali zao, alijali utu na heshima hii ndiyo
sababu na mimi alikuwa rafiki yangu,” alieleza Rais Kikwete.
Alibainisha kwamba licha ya kuwa Muislamu mara
kadhaa Askofu huyo alifika kumwombea Ikulu na katika maombezi yake
alisisitiza kuwa alikuwa akiwaombea Watanzania na nchi nzima kwa ujumla,
hivyo aliwahimiza walio hai kumuenzi Askofu kwa vitendo.
Kwa upande wake, Makamu Askofu Mkuu wa EAGT
Asumwisye Mwaisabila, akizungumzia msiba huo kuwa marehemu Kulola
alikuwa mchungaji wa aina yake na hivyo kuwataka wanaotaka kufanana naye
kuomba kwa Mungu awajalie hekima.
“Alikuwa askofu wa ajabu sana, hata kama ungeweza
kumtandikia mkeka ili alale, angelala. Jambo hili ni tofauti sana na
maaskofu wa kileo ambao ukiwatendea hivyo watanung’unika na kukusema
kila siku,” alieleza na kusisitiza wanapaswa kumuenzi kwa vitendo.
Katika Ibada ya maziko ya Askofu Kulola
iliyoongozwa na Makamu Askofu Mkuu, Asumwisye Mwaisabila, mbali na Rais
Kikwete pia Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Dk Willibroad Slaa, aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, Wabunge William Ngeleja (Sengerema),
Ezekiel Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela) pamoja na Mchungaji
Peter Msigwa, ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini.
Wakati huohuo Rais Kikwete jana alisafiri kwenda Kampala, Uganda, kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
No comments:
Post a Comment