Makubwa zaidi yafichuka dawa za kulevya
Mhadhiri na Mtaalamu wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo
Kwa ufupi
Mitaani vijana wanasikika wakisifia bangi
inayouzwa na Khamis (siyo jina lake halisi). Wanashawishiana kwenda
kununua kwa mtu huyo wakisifu kuwa ina ‘stimu’ nzuri isiyokwisha haraka
tofauti na za mtu mwingine (wanamtaja kwa jina).
Kwa yule ambaye si mzoefu wa kutumia vilevi hivi
huwezi kuuziwa, kwani kuna ishara ambazo hupeana ili kujua kama huyu ni
mnunuaji au polisi.
Zipo ishara mbalimbali wanazozitumia wakati wa
kununua bangi hizi, mfano ukiwa na gari usiku utatakiwa kuzima taa za
nje na kuwasha za ndani. Muuzaji akiona hivyo tu anajua kuwa aliyefika
ni mteja wake.
Aidha hata namna wanavyopeana pesa ni tofauti,
muuzaji hakabidhiwi mkononi badala yake unaiweka tu kwenye kiti cha
gari, naye akifika anaweka mzigo chini na kuchukua pesa yake.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua
kuwa, huu ndiyo mwanzo wa watumiaji wa bagi kuingia katika matumizi ya
dawa za kulevya.
Aidha hata namna wanavyopeana pesa ni tofauti,
muuzaji hakabidhiwi mkononi badala yake unaiweka tu kwenye kiti cha
gari, naye akifika anaweka mzigo chini na kuchukua pesa yake.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua
kuwa, huu ndiyo mwanzo wa watumiaji wa bangi kuingia katika matumizi ya
dawa za kulevya.
Wauza dawa za kulevya matajiri nchini, wanafanya
hila kuhakikisha vijana wadogo wanaingia kwenye utumiaji wa dawa za
kulevya, ili watengeneze wateja endelevu wa biashara yao.
Inasemekana kuwa kauli mbiu wanayoitumia ni ‘Get
Them While They’re Young’, wakimaanisha kuwa wawaingize kwenye matumizi
ya dawa za kulevya wakati wakiwa bado wadogo, ili wanapofikia umri wa
kuingiza kipato wawafaidishe wao kwa kununua ‘unga’.
Uchunguzi unaonyesha kuwa matajiri hawa wakati
mwingine huwalipa wauza bangi na kuwapa dawa za kulevya bure, ili
wazichanganye wakiamini kuwa wanatengeneza wateja wengi kwa wakati
mmoja.
Kwa wasiovuta bangi wamekuwa wakichanganyiwa
katika sigara na matendo kama haya hufanyika zaidi katika klabu za usiku
na waathirika wakubwa wa njia hii ni wasichana.
“Wasichana hudanganywa na wapenzi wao wakiambiwa
vuta kidogo, ni nzuri nao hujikuta wakijaribu na kurudia tena kwa kuwa
kile wanachovuta si sigara ya kawaida, mwisho wa siku huingia kwenye
‘uteja’” kinasema chanzo cha habari.
No comments:
Post a Comment