Mbunge ajitoa ujumbe bodi ya CDA kupinga bomoabomoa

NA JACQUELINE MASSANO
Mbunge wa Dodoma Mjini, David Malolle (CCM), ametangaza rasmi kujitoa kwenye ujumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na kuwataka wananchi kuandamana ili mamlaka hiyo ifutwe kwani imekuwa ikibomoa mji na si kuuboresha.(hd)
Mbunge wa Dodoma Mjini, David Malolle (CCM), ametangaza rasmi kujitoa kwenye ujumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na kuwataka wananchi kuandamana ili mamlaka hiyo ifutwe kwani imekuwa ikibomoa mji na si kuuboresha.(hd)
Mbunge
huyo alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya
Chang'ombe Magharibi mara baada ya uzinduzi wa ofisi ya tawi la kata
hiyo.
"Mimi binafsi sioni sababu ya kuendelea kuwapo ndani ya bodi hiyo wakati wananchi wangu wanaendelea kunyang'anywa mashamba, viwanja na kuvunjiwa nyumba bila sababu za msingi," alisema na kuongeza:
"Mimi binafsi sioni sababu ya kuendelea kuwapo ndani ya bodi hiyo wakati wananchi wangu wanaendelea kunyang'anywa mashamba, viwanja na kuvunjiwa nyumba bila sababu za msingi," alisema na kuongeza:
"Hata CDA
inapochukua eneo kubwa la mwananchi wangu hawako tayari kumuachia
viwanja zaidi ya kimoja na wala fidia hawawalipi sasa kwa nini mimi
niendelee kukaa ndani ya hiyo bodi."
Malolle
alisema licha ya kuwapo katika bodi hiyo, lakini ushauri wake umekuwa
ukipuuzwa, hivyo haoni sababu ya kuendelea kuwapo ndani ya bodi. Alisema
kutokana na kuendelea kwa hali hiyo ni muhimu sasa wananchi wa meeneo
yote wanaotishiwa kuvunjwa na mamlaka hiyo kuandamana ili kuhakikisha
bodi hiyo inavunjwa.
Aidha,
alisema kutokana na yeye kutokuwa mjumbe tena kwenye bodi hiyo, yupo
tayari kukunjua makucha ili kuhakikisha CDA inafanya kazi iliyokusudiwa
na si vinginevyo.
"Kusudio
la serikali kuanzisha Bodi hiyo ni kuhakikisha kuwa mji wa Dodoma
unaboreshwa na si kubomolewa na wenyeji kuhamishwa kwa madai ya kupanga
mji...sasa kama kazi ya CDA ni kubomoa mji kwa kisingizio cha ujenzi wa
makao makuu, nawaomba wakazi wenzangu wa Nzunguni, Miyuji na sehemu
zingine tuungane pamoja tuandamane kuipinga mamlaka hii," alisema.
Kwa
mujibu wa mbunge huyo, CDA imekuwa ikivunja sehemu mbalimbali na
wanapoulizwa na wananchi hudai kuwa wakamuulize mbunge kwani ni mjumbe
wa bodi ambaye anajua kilichoamuriwa, jambo ambalo alisema siyo kweli.
Naye,
Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Albert Mgumba, alisema wale wote wanaoleta
msuguano ndani ya chama wakati wa chaguzi watolewe mapema. Alisema
sehemu nyigi ambazo CCM ilikosa udiwani au ubunge katika chaguzi
zilizopita kulisababishwa na wana-CCM wenyewe, hivyo hakuna sababu ya
kuwalea watu wa aina hiyo.
"CCM
ndiyo chama pekee ambacho kimeweza kutunza amani na utulivu katika
kipindi chote cha Uhuru wa Tanzania... bila nia njema ya waasisi wa nchi
akiwamo Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na Karume, amani iliyopo hivi
sasa isingekuwapo," alisema.
No comments:
Post a Comment