Askari wakiutoa mwili wa marehemu jioni hii katika kichaka juu ya mawe ambapo ndipo ulipotupwa(Picha Na George Almas)
Askari wakiupakia mwili wa marehemu huku wananchi walio na huzuni wakishuhudia
(Picha Na George Almas)
Katika hali ya kuhuzunisha ni kwamba
maiti iliyokuwa imewekwa ndani ya mfuko(kisalufeti) imekutwa imetupwa
maeneo ya jirani kabisa na chuo kikuu cha Tumaini Iringa(University of
Iringa). Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa maiti hiyo imeonekana
baada ya kuhisi harufu mbaya ikitokeo jirani kabisa na makazi yao, baada
ya kuhisi harufu hiyo walianza kutaka kujua harufu inatoka wapi na
inatokana na nini ndipo walipo fika eneo hilo na kukuta mwili huo ukiwa
ndani ya mfuko. Wananchi hao wanasema maiti hiyo imeharibiaka sana.
lakini mpaka sasa haijajulikana kuwa maili huyo ni nani. Baada ya kuona
mwili huo wananchi walitoa taarifa polisi ambao walifika na kuuchukua
mwili wa marehemu.(P.T)
Picha Na George Almas
No comments:
Post a Comment