Boko Haram waua madereva 19 Nigeria
Wanamgambo waliokuwa wamevaa nguo za
kijeshi, wamewaua watu 19 katika kuzuizi cha barabarani walichokuwa
wameweka kukagua magari katika jimbo la Borno.
Mabaki ya magari ya madereva waliouawa na Boko Haram
Wanaume hao waliokuwa wamejihami ,
waliwasimamisha madereva na kuwaamrisha kuondoka kutoka katika magari
yao kabla ya kuwapiga risasi na kuwaua.
Walioshuhudia tukio hilo waliambia BBC
kuwa wanaume hao walikuwa wanachama wa Boko Haram, ingawa kundi hilo
bado halijatamka chochote kuhusu mauaji hayo.
Jimbo hilo la Kaskazini mwa Nigeria
liko chini ya sharia ya hali ya hatari, huku Boko Haram wakiwa vitani na
serikali kutaka utawala wa kiisilamu.(P.T)
Kundi hilo huwalenga raia na wanajeshi kwa mashambulizi ikiwemo shule na makabiliano ya mara kwa mara na jeshi la taifa.
Shambulizi la hivi karibuni,
lilifanyika Jumapili, asubuhi karibu na mji wa Logumani, ambao hauko
mbali sana na mpaka na Cameroon.
Walionusurika shambulizi hilo walisema
kuwa washambuliaji walivaa nguo za jeshi na walikuwa wanaendesha
pikipiki kabla ya kuwashambulia waathiriwa.
"Takriban wanaume 9 walituamuru kuondoka kwenye magari yeu na kulala chini,'' alisema mwanamume
"Waliwaua watu 5 kwa kuwapiga risasi
na kasha kuwanyonga wengine 14 kabla ya mtu mmoja kuwapigia simu na
kuwambia kuwa wanjeshi wanakuja.''
Alisema washambuliaji baadaye walitoroka na kujificha msituni kwa pikipiki zao.
Manusura mwingine alisema kuwa
alisikia mtu aliyekuwa karibu naye akiuawa kwa kisu. Alisema ana uhakika
kuwa washambuliaji walikuwa Boko Haram kwa sababu ya kuwa na ndevu.
Mwandishi wa BBC Tomi Oladipo alisema
kuwa ni jambo la kawida kwa polisi kuweka vizuizi barabarani hasa katika
maeneo yenye misukosuko na huenda washambuliaji waliiga mbinu hioyo ya
jeshi ili kuwanasa waathiriwa. I,
Boko Haram limezua mgogoro mkubwa wa
kisiasa Nigeria tangu mwaka 2009, nia yao kuu ikiwa kuunda utawala wa
kiisilamu, hasa katika maeneo ya kaskazini mwa nchi
Kundi hilo limelaumiwa kwa mashambulizi kadhaa ambao yamesababisha takribna vifo 2,000 tangu mwka 2011.