Pages

Wednesday, 4 September 2013


Mandela arudishwa nyumbani

Gari la kubebea wagonjwa likimrudisha nyumbani Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela jana
JOHANNESBURG, Afrika Kusini
SERIKALI ya Afrika Kusini imesema kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Nelson Mandela, ametolewa hospitali ambako amekuwa akitibiwa ugonjwa wa mapafu tangu Juni mwaka huu.
 
endelea...
Taarifa hiyo imekuja siku moja baada ya maofisa wa nchi hiyo kukanusha habari zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo kuwa Mandela (95) ameruhusiwa kutoka hospitalini.
Kwa mujibu wa taarifa katika tovuti ya Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, imeeleza kuwa Mandela bado ni mahtuti na hali yake wakati mwingine inabadilika Lakini madaktari wake wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale ya hospitali.
Nyumba ya Mandela imebadilishwa ili kumruhusu kupata matibabu ya mgonjwa mahtuti akiwa nyumbani.
Serikali imesema inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu.

No comments: