LEMA KUIVURUGA CCM MBALIZI
Na kelvin Lameck Mbeya
MBUNGE wa
Arusha mjini Godbless Lema (Chadema), anatarajia kufanya mkutano wa kihistoria
katika mji wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini jumapili Julai 21, mwaka huu.
Akizungumza
na Mtandao wa kalulunga blog, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo
Kissman Mwangomale (KK)(Chadema) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha
Mshikamano kata ya Nsalala, alisema kuwa mkutano huo utafanyika katika viwanja
vya mahubiri vilivyopo Tazara mjini hapo.
Alisema
ziara hiyo ya Lema imeandaliwa na kata mbili ambazo ni kata ya Utengule Usongwe
na kata ya Nsalala zote za mjini Mbalizi.
‘’Mkutano
huo unalenga kuimarisha chama na kudhihilisha kuwa kauli ya Rais Jakaya Kikwete
aliyosema kuwa sisi ni vyama vya msimu si kweli, bali tunao uwezo wa kuimarisha
chama kila wakati’’ alisema Mwangomale.
Alisema
chama chake ndicho kinaongoza katika vijiji vya Mbalizi kata ya Ytengule
Usongwe na Kijiji cha Mshikamano kata ya Nsalala ambako ni mahala panapoonekana
kuwa na vuguvugu kubwa la kisiasa na makao makuu ya siasa za wilaya ya Mbeya
vijijini.
‘’Mbali na
Mbunge Lema, wabunge wengine ambao tumewaalika ni pamoja na Mbunge wa Mbozi
Magharibi David Silinde, Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mbunge wa Iringa
mjini Mchungaji Peter Msigwa’’ alisema Mwangomale.

No comments:
Post a Comment