Pages

Tuesday, 30 July 2013

Jaji Werema akerwa wapelelezi kubambikia watu kesi mbaya

 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema  

Na Kelvin Lameck
Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, amewataka wapelelezi wa makosa ya jinai nchini, kutowabambikia watu kesi kwa nia ya kulipiza visasi na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Endelea......
Jaji Werema aliyasema hayo jana wakati akizungumza na mawakili wafawidhi na wakuu wa upelelezi wa kesi za jinai wa mikoa na vikosi vingine vya polisi mjini Dodoma.
Alisema kuna malalamiko kuhusu askari wa upelelezi kuwabambikia kesi mbaya watu wasiokuwa na hatia na kuwataka waache mara moja tabia hizo.
“Hakikisheni kuwa mnafanya kazi zenu kwa weledi na siyo kuwabambikia watu wasiokuwa na hatia kesi mbaya na wengine hadi kesi za mauaji kwa sababu tu una kisasi naye. Hili ni kosa kubwa la jinai na tukikubaini tutakuchukulia hatua kali za kisheria,” alisema Jaji Werema.
Hata hivyo aliwataka wapelelezi hao kuharakisha upelelezi wa makosa ya jinai, ili kuondokana na tabia ya kuwakamata watu wasio kuwa na hatia.
“Kila inapowezekana chunguzeni tuhuma haraka kabla ya kumkamata mtuhumiwa ili kuepuka kauli za upelelezi bado haujakamilika,” alisema Jaji Werema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka, Dk Elieza Feleshi, aliwataka wajumbe wa mkutano huo kutumia nafasi hiyo kutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Alisema wasipofanya kazi kwa pamoja, jukumu la kulinda na kudumisha amani iliyopo hapa nchini, litawashinda.
“Wahalifu wanaohatarisha amani hapa nchini wautumie vizuri muda wa wiki mbili walizopewa na Rais Jakaya Kikwete vinginevyo watakumbana na mkono wa sheria na kujutia vitendo vyao viovu wanavyovifanya,” alisema Dk Feleshi.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakiwalalamikia polisi wa upelelezi kuwabambikia kesi kama njia ya kuwashinikiza kutoa rushwa au kulipiza visasi.
Tatizo hilo pia limelalamikiwa na wanaharakati wa haki za binadamu ambao mara kadhaa wamekuwa wakiitaka Serikali kuchukua hatua za kuwashughulikia askariwa aina hiyo.
Mara kadhaa viongozi wa polisi kwa upande wao, nao wamekuwa wakiahidi kuchukua hatua dhidi ya askari hao wasioku

No comments: