Pages

Thursday, 18 July 2013

habari mikoani

Morogoro
Na Kelvin Lameck

 ABIRIA 23 wa basi la Kampuni ya Air lililokuwa likisafiri kutoka mkoani Tabora kuelekea Dar es Salaam wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea juzi, majira ya saa 11:15 jioni maeneo ya Maseyu, Tarafa ya Mikese na idaiwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa basi hilo. Kati ya majeruhi hao 19 wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na wanne wamepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kuumia vibaya.

Tanzania Daima ilishuhudia majeruhi wa basi hilo T 513 BRT Scania, wakiwasili katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro huku wengi wao wakiwa wamejeruhiwa kichwani na mikononi.

Baadhi ya majeruhi waliozungumza na Tanzania Daima walisema dereva wa basi alikuwa akijaribu kuyapita magari matatu yaliyokuwa mbele yake na ndipo ghafla aliona basi likija mbele yake, hivyo kukwepa kugongana nalo uso kwa uso kwa kwenda pembeni.

Walisema hali hiyo ilisababisha basi hilo kuingia kwenye gema na kupinduka.

No comments: