‘Mtanzania’ akamatwa kesi ya utumwa Uingereza
Polisi wakiwa nje ya moja kati ya majengo yanayohisiwa kutumika kama
makazi ya mke na mume waliokamatwa Alhamisi kwa tuhuma za kujihusisha na
utumwa. Mmoja kati ya watuhumiwa hao ametokea Tanzania. PICHA | LEON
NEAL-AFP
London.
Mmoja kati ya watuhumiwa wawili wanaoshutumiwa kuwashikilia wanawake
watatu katika mazingira ya utumwa kwa miaka 30 mjini London anatokea
Tanzania, polisi Uingereza wamesema Jumamosi.

