Jaji Werema akerwa wapelelezi kubambikia watu kesi mbaya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema
Na Kelvin Lameck
Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, amewataka wapelelezi wa makosa ya jinai nchini, kutowabambikia watu kesi kwa nia ya kulipiza visasi na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Endelea......
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, amewataka wapelelezi wa makosa ya jinai nchini, kutowabambikia watu kesi kwa nia ya kulipiza visasi na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Endelea......
Jaji Werema aliyasema hayo jana wakati akizungumza
na mawakili wafawidhi na wakuu wa upelelezi wa kesi za jinai wa mikoa
na vikosi vingine vya polisi mjini Dodoma.
Alisema kuna malalamiko kuhusu askari wa upelelezi
kuwabambikia kesi mbaya watu wasiokuwa na hatia na kuwataka waache mara
moja tabia hizo.
“Hakikisheni kuwa mnafanya kazi zenu kwa weledi na
siyo kuwabambikia watu wasiokuwa na hatia kesi mbaya na wengine hadi
kesi za mauaji kwa sababu tu una kisasi naye. Hili ni kosa kubwa la
jinai na tukikubaini tutakuchukulia hatua kali za kisheria,” alisema
Jaji Werema.
Hata hivyo aliwataka wapelelezi hao kuharakisha
upelelezi wa makosa ya jinai, ili kuondokana na tabia ya kuwakamata watu
wasio kuwa na hatia.
“Kila inapowezekana chunguzeni tuhuma haraka kabla
ya kumkamata mtuhumiwa ili kuepuka kauli za upelelezi bado
haujakamilika,” alisema Jaji Werema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mashtaka, Dk Elieza
Feleshi, aliwataka wajumbe wa mkutano huo kutumia nafasi hiyo kutatua
changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo kwenye utekelezaji wa majukumu
yao ya kila siku.
Alisema wasipofanya kazi kwa pamoja, jukumu la kulinda na kudumisha amani iliyopo hapa nchini, litawashinda.
“Wahalifu wanaohatarisha amani hapa nchini
wautumie vizuri muda wa wiki mbili walizopewa na Rais Jakaya Kikwete
vinginevyo watakumbana na mkono wa sheria na kujutia vitendo vyao viovu
wanavyovifanya,” alisema Dk Feleshi.
Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na
malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wakiwalalamikia polisi wa upelelezi
kuwabambikia kesi kama njia ya kuwashinikiza kutoa rushwa au kulipiza
visasi.
Tatizo hilo pia limelalamikiwa na wanaharakati wa
haki za binadamu ambao mara kadhaa wamekuwa wakiitaka Serikali kuchukua
hatua za kuwashughulikia askariwa aina hiyo.
Mara kadhaa viongozi wa polisi kwa upande wao, nao
wamekuwa wakiahidi kuchukua hatua dhidi ya askari hao wasioku
No comments:
Post a Comment