Pages

Tuesday, 30 July 2013

WAZIRI MKUU WA THAILAND AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA SIKU 3

Picha na 5 8a80a
Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam

Na Meck Lameck

Jaji Werema akerwa wapelelezi kubambikia watu kesi mbaya

 

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema  

Na Kelvin Lameck
Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, amewataka wapelelezi wa makosa ya jinai nchini, kutowabambikia watu kesi kwa nia ya kulipiza visasi na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri Sitta: Kuna wabunge mizigo CCM


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta 
Na Kelvin Lameck


Busega. Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amesema baadhi ya wabunge wa CCM ni mizigo kwani hata wakienda bungeni, hawachangii na wanabebwa na chama.


 
WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA 
CIMG8390 44a58

MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa.

Yusufu Amani (39) aliyembaka mwanaye wa kumzaa kisha kumzalisha baada ya kutengana na mkewe Afungwa miaka 30
Hapa akijifunika sipigwe picha baada ya hukumu
Kulia ni mtoto aliyebakwa na baba yake kisha kuzalishwa akiwa na mtoto wake wakitoka mahakamani kulia ni mama mzazi wa binti aliyebakwa na kuzalishwa
Na kelvin Lameck

MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 30 mkazi wa Isanga Mkoani hapa baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti na kumzalisha binti yake wa kumzaa akiwa na miaka 15( jina linahifadhiwa).

Saturday, 27 July 2013

JK azidi kuwasha moto


Rais Jakaya Kikwete
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 *Atangaza wiki mbili msako wa silaha mikoa mitatu
*Asema wakishindwa JWTZ, Polisi wataingia kazini

RAIS Jakaya Kikwete, ametangaza msimamo mkali baada ya kutoa wiki mbili kwa watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma kuzisalimisha kwa hiari yao kabla ya kutiwa mbaroni.

Tuesday, 23 July 2013


 WAHIMIZWA KUHUBIRI AMANI,UPENDO
Na kelvin Lameck
 
 Viongozi wa madhehebu ya dini wametakiwa kuhakikisha wanadumisha utulivu uliopo nchini kwa kuhubiri amani na upendo kwa watu wote

Wajane JWTZ waililia Serikali 

Na Kelvin Lameck 

Sura za Habari Hii
Wajane JWTZ waililia Serikali
Chanzo cha vifo
MIILI YAWASILI UPANGA
Rambirambi

*Wataka Serikali iwajengee nyumba, isomeshe watoto
*JK kupeleka ombi UN, AU sheria zibadilishwe

Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakitoa heshima za mwisho jijini Dar es Salaam jana kwa miili ya askari wenzao waliouawa Darfur, Sudan, wiki iliyopita. Picha na Anthony Siame

WAZEE 292 WAPATIWA VITAMBULISHO VYA MATIBABU

Kushoto ni Afisa mtendaji kata ya Utengule Usongwe wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani MBEYA,  John Mwanampazi, akiwa na Afisa Maendeleo ya Jamii kata hiyo Martin Gowele wakizungumza na mwandishi wa habari.


Kitambulicho cha matibabu kwa wazee waliofikisha miaka 60 na zaidi.
Na, Kelvin Lameck, Mbalizi

Saturday, 20 July 2013

AJALI MBAYA DODOMA

 WATU wanne wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Najimunisha lililokuwa likitokea Dar es Saalam kwenda Mwanza kupasuka tairi la mbele na Kupinduka katika eneo la Mbande Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma LEO.

Friday, 19 July 2013


Mchungaji adaiwa kulawiti watoto 3

*Baba naye ambaka mwanae usiku

Na Kelvin Lameck
JESHI la Polisi Kituo cha Stakishari Ukonga jijini Dar es Salaam linamshilikia kwa uchunguzi Mchungaji wa Kanisa moja la Kilokole (jina tunalihifadhi) kwa tuhuma za kuwalawiti kwa nyakati tofauti watoto watatu.
Mbali ya mchungaji huyo kushikiliwa katika kituo hicho, wapo watuhumiwa wengine wawili mmoja akiwa ni mdogo wake mtumishi huyo wa Mungu na msichana aliyekuwa akiwapeleka watoto hao kufanyiwa unyama huo.   Vitendo hivyo vinadaiwa vimekuwa vikifanywa na mchungaji huyo kwa nyakati tofauti maeneo ya Ukonga Moshi Bar jijini Dar es Salaam.

viboko

WAZAZI WAWAVAMIA WALIMU NA KUWACHAPA VIBOKO HUKO MOROGORO BAADA YA KUCHOSHWA NA VITENDO VYAO VYA KUWATESA WANAFUNZI..!!


Shukuru Kawambwa,Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi.                                                              


Kundi la wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya Msingi Kinole, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, mkoani Morogoro, wamevamia shule hiyo na kuwachapa walimu bakora na kusababisha baadhi yao (walimu) kujeruhiwa.

chadema

RUVUMA

Chadema kutumia anga katika Mabaraza ya Katiba

 
Akizungumza juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Stendi ya Malori, Majengo mjini Songea, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema utaratibu wa chama hicho kujadili maoni hayo utatolewa hivi karibuni.
Alisema wamekuwa na dhamira ya kuona Watanzania wanapata katiba inayotokana na matakwa yao kwa ajili ya kusimamia na kulinda masilahi yao, hivyo chama chake hakitafanya mikutano ya ndani au ya siri.

Thursday, 18 July 2013

habari mikoani

Morogoro
Na Kelvin Lameck

 ABIRIA 23 wa basi la Kampuni ya Air lililokuwa likisafiri kutoka mkoani Tabora kuelekea Dar es Salaam wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea juzi, majira ya saa 11:15 jioni maeneo ya Maseyu, Tarafa ya Mikese na idaiwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa basi hilo. Kati ya majeruhi hao 19 wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na wanne wamepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kuumia vibaya.

Tanzania Daima ilishuhudia majeruhi wa basi hilo T 513 BRT Scania, wakiwasili katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro huku wengi wao wakiwa wamejeruhiwa kichwani na mikononi.

Baadhi ya majeruhi waliozungumza na Tanzania Daima walisema dereva wa basi alikuwa akijaribu kuyapita magari matatu yaliyokuwa mbele yake na ndipo ghafla aliona basi likija mbele yake, hivyo kukwepa kugongana nalo uso kwa uso kwa kwenda pembeni.

Walisema hali hiyo ilisababisha basi hilo kuingia kwenye gema na kupinduka.

SOKO JIPYA MWANJELWA UTATA



na Kelvin Lameck, Mbeya
MRADI mkubwa wa ujenzi wa Soko jipya la Mwanjelwa ulioanza baada ya soko lililokuwapo kuteketezwa kwa moto mwaka 2006, umekwama kumalizika kutokana na mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kuishiwa fedha.

Uchunguzi wa umebaini kukwama kwa ujenzi wa soko hilo katika hatua za mwisho huku timu ya wataalamu kutoka Benki ya CRDB iliyotoa mkopo wa sh bilioni 13 wakihaha kufuatilia deni lao.

Benki ya CRDB iliikopesha Halmashauri ya Jiji la Mbeya fedha hizo ili kufanikisha ujenzi wa soko hilo na mkopo ulitakiwa utumike ndani ya miaka mitano na baada ya hapo jiji hilo lianze kurejesha mkopo huo na riba.

Kushindwa kukamilika kwa soko hilo ambalo ni kitega uchumi kikubwa katika halmashauri ya jiji hilo kumeibua hisia tofauti huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia uzembe uliofanywa na mkandarasi, Kampuni ya Tanzania Building Works Ltd (TBWL).

Mkurugenzi wa Tawi la CRDB Mbeya, Benson Mwakyusa, alisema ingawa si msemaji alikiri kupokea ugeni kutoka CRDB makao makuu na kwamba walikuwa na jukumu la kufuatilia masuala mengine ya kikazi na kukutana na mkopaji ambaye ni halmashauri ya jiji hilo, ili kuangalia njia nyingine ya kukamilisha ujenzi wa soko hilo.

Mhandisi mshauri wa ujenzi wa soko hilo, Dudley Mawalla, kutoka Kampuni ya MD Consultancy Limited alipohojiwa ili aeleze hali iliyosababisha ujenzi wa soko hilo usimame, naye aliruka na kudai kuwa si msemaji na anayetakiwa kusema ni mmiliki wa soko hilo ambao ni Jiji la Mbeya.

Mkurugenzi wa jiji hilo, Musa Zungiza, alikiri mkandarasi aliyepewa kazi ya ujenzi wa soko kushindwa kumalizia ujenzi licha ya kuomba aongezewe muda ambao nao ulimalizika na ndipo walipogundua kuwa aliishiwa fedha na ameshindwa pia kutimiza masharti waliyokubaliana.

“Sisi kama jiji hatumdai hadi pale alipofikia, kweli alituomba fedha, tulimuomba atupatie mpango mzima wa kazi na mtiririko wa fedha kutoka benki, tumefikia mahali tumekosana kwa kuwa hajatimiza masharti na tumezungumza na mhandisi mshauri ili tuone jinsi ya kumpata mkandarasi mwingine,” alisema Zungiza.

  Mbeya

TAMASHA LA INJILI KUWEKA HISTORIA MBEYA


TAMASHA kubwa la muziki wa injili linalotarajiwa kufanyika ukumbi wa Kanisa la Pentekoste Holiness Association Mission (Makimbilio), karibu na lango kuu la Shule ya Sekondari Samora, Mbeya Agosti 4, mwaka huu, linatarajiwa kuweka historia mpya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa tamasha hilo, George Kayala alisema kuwa, wasanii mbalimbali wa Bongo Movie wakiongozwa na pacha wa muigizaji wa filamu na muziki, Husna Posh 'Dotnata', Dometria Alphonce 'DD' wameandaa kitu kwa ajili ya wakazi wa Mbeya.

“Tamasha hilo litakuwa ni la kihistoria, kwani litapambwa na wasanii wa filamu nchini wakiongozwa na pacha wa Dotnata na watakuwa na jambo la kusema na watu watakaofika katika tamasha hilo,” alisema Kayala.

Kayala alisema kuwa tamasha hilo limeandaliwa na GMK Production kwa ajili kuitambulisha albamu ya tatu ya ‘Nitang’ara Tu’ ya Mwinjilisti Kabula George, ikiwa katika mfumo wa DVD na siku hiyo itauzwa kwa wakazi wa Mbeya.

Kiingilio katika tamasha hilo ni sh 2,000 kwa watu wazima na 1,000 kwa watoto na shughuli itaanza saa 7:00 mchana na kumalizika saa 12:00 jioni.

“Tumeamua kuweka kiingilio kidogo ili kila mmoja apate kuingia katika tamasha hilo, ambalo litakuwa la kwanza kuwakutanisha nyota wa filamu na waimbaji wa nyimbo za injili mkoani humo,” alisema Kayala.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Ushindi Redio FM ya Mbeya, Shalom Production, DD Entertainment, The Genesis Global College na Dotnata Entertainment.

UFISADI JIJI LA MBEYA, KANUNI NDOGO ZA JIJI ZILIZOSAINIWA NA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ZASHINDWA KUSIMAMIWA.

Meya Jiji la Mbeya Athanas Kapunga

By Kelvin Lameck

lema

LEMA KUIVURUGA CCM MBALIZI



  Godbless Lema
Na kelvin Lameck Mbeya
MBUNGE wa Arusha mjini Godbless Lema (Chadema), anatarajia kufanya mkutano wa kihistoria katika mji wa Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini jumapili Julai 21, mwaka huu.
Akizungumza na Mtandao wa kalulunga blog, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo Kissman Mwangomale (KK)(Chadema) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mshikamano kata ya Nsalala, alisema kuwa mkutano huo utafanyika katika viwanja vya mahubiri vilivyopo Tazara mjini hapo.
Alisema ziara hiyo ya Lema imeandaliwa na kata mbili ambazo ni kata ya Utengule Usongwe na kata ya Nsalala zote za mjini Mbalizi.
‘’Mkutano huo unalenga kuimarisha chama na kudhihilisha kuwa kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyosema kuwa sisi ni vyama vya msimu si kweli, bali tunao uwezo wa kuimarisha chama kila wakati’’ alisema Mwangomale.
Alisema chama chake ndicho kinaongoza katika vijiji vya Mbalizi kata ya Ytengule Usongwe na Kijiji cha Mshikamano kata ya Nsalala ambako ni mahala panapoonekana kuwa na vuguvugu kubwa la kisiasa na makao makuu ya siasa za wilaya ya Mbeya vijijini.
‘’Mbali na Mbunge Lema, wabunge wengine ambao tumewaalika ni pamoja na Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde, Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa’’ alisema Mwangomale.