Pages

Sunday, 20 October 2013

Utafiti wabashiri Katiba mpya

WAKATI Tume ya Mabadiliko ya Katiba ikiandaa rasimu ya pili ya Katiba itakayopelekwa katika Bunge la Katiba, utafiti uliofanywa na asasi ya kimataifa umebashiri baadhi ya matokeo ya Katiba ijayo.

Wednesday, 16 October 2013

Samaki wabovu waielemea Serikali

 
Msemaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Roida Andusamile amekiri kuwa shirika hilo lilikutana na samaki hao kabla hawajaletwa nchini. PICHA|MAKTABA 

Tuesday, 15 October 2013

Mama yake Ufoo alipigwa risasi tano


TAARIFA zaidi za kusikitisha kuhusu mauaji ya kinyama, yaliyofanyika katika familia ya Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro zimeendelea kutolewa, ambapo imebainika mama mzazi wa mtangazaji huyo, Anastazia Saro (58), aliuawa kwa kupigwa risasi tano.

GARI LA MWISHO KUTUMIWA NA MAREHEMU BABA WA TAIFA,NA MAGARI MENGINE YA SERIKALI ALIYOKUWA AKIYATUMIA ENZI ZA UHAI WAKE

Mwalimu kambarage
Hili ni gari ambalo marehemu baba wa Taifa ambae leo anatimiza miaka 14 tangu kufariki kwake alilitumia wakati anapelekwa Airport kwaajili ya matibabu.

Hali ya muandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro inaendelea vizuri.

Hali ya muandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro aliyejaruhiwa kwa risasi na mzazi mwenzie inaendelea vizuri lakini bado yupo chini ya uangalizi maalum wa madaktari.

Kwa mujibu wa madaktari waliomfanyia upasuaji wa kuondosha risasi iliyokuwa tumboni Ufoo anahitaji muda mwingi wa kupumzika ili aweze kupata nafuu na kurudi katika hali yake ya kawaidia.



Muandishi huyo alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Tumbi Kibaha Mkoani Pwani ambapo alipelekwa mara baada ya kukutwa na tukio hilo.

Wednesday, 9 October 2013

Wawekezaji wanyanyasaji kufukuzwa


SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema wawekezaji watakaobainika kujishughulisha na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia pamoja na kuwasumbua wafanyakazi katika sekta za mahoteli watachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa nchini.

Mfanyabiashara Arusha adai kumwagiwa tindikali


MFANYABIASHARA Japhet Minja amelazwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Centre (Seliani) jijini Arusha, baada ya kumwagiwa kimiminika kinachosadikiwa kuwa tindikali usoni na watu wasiojulikana.