Pages

Monday, 23 September 2013

DCI Manumba: Tumejiandaa

 
 

Kwa ufupi
  • Alipotakiwa kutoa msimamo wa jeshi hilo iwapo taarifa hizo zitakuwa na ukweli alisema, “Jeshi tuko tayari kwa jambo lolote.”

JOHNSON JABIR MWANDISHI HABARI AVAMIWA, APIGWA NA MAPANGA, AJERUHIWA

ARUSHA: (JAIZMELALEO) - Maisha ni safari ndefu wadau wa JAIZMELALEO.
Siku zote mshukuru Mungu kwa kila jambo linapotokea katika maisha yako wala usiwe na hofu kabisa hata kama linauma kama nini LEAVE TO GOD.
Usiku wa kuamkia Septemba 22, 2013 katika mtaa wa Elkurei katika Kata ya Kiranyi, Arumeru mkoani Arusha wezi walinivamia na kunijeruhi haswa.
Walibeba vifaa vya kazi lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kunitoa roho lakini Mwenyezi Mungu alininusuru kwa kunitia nguvu kupambana nao walikunja na marungu, visu na mapanga.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE KWA YOTE.

Sunday, 22 September 2013

39 wauawa madukani Kenya, Al-Shabab yakiri kuhusika

Polisi wa Kenya akimuokoa mtoto, baada ya kundi la watu waliokuwa  na silaha kuvamia duka kubwa la bidhaa katika jengo la Wastgate, jijini Nairobi, jana na kuwaua zaidi ya 20 na wengine kuwajeruhi.
Kwa ufupi

Sunday, 8 September 2013

Kibano chamgeukia Ndugai 



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
*Yadaiwa alipewa maelekezo kuwabana wapinzani
*Profesa Lipumba adai uwezo wake bungeni mdogo

NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amezidi kujiweka katika wakati mgumu, baada ya viongozi wa vyama vya upinzani kudai alipewa maelekezo na Serikali kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba. Kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), walisema ni wazi, Ndugai ameonekana kuwa na uwezo mdogo wa kuongoza Bunge, kutokana na kusababisha vurugu kubwa ndani ya ukumbi wa Bunge wiki iliyopita.

Mtoto amkatakata mamaye kinyama

Na Lilian Mkusa, Njombe
WIKI iliyopita katika Mtaa wa Maheve uliopo Kata ya Ramadhani mkoani Njombe yalitokea mauaji ya kutisha yanayomhusisha mtoto aliyemkatakata mama yake mzazi kwa shoka kutokana na kugombania mirathi.

Wazanzibari waliumbua Bunge

Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal(kulia), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki mara baada ya kufungua Kongamano la Katiba Mpya na Nafasi ya Wazenjibara (Wazanzibari wanaoishi bara)

Makubwa zaidi yafichuka dawa za kulevya

Mhadhiri na Mtaalamu wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo 
Kwa ufupi
Kwa yule ambaye si mzoefu wa kutumia vilevi hivi huwezi kuuziwa, kwani kuna ishara ambazo hupeana ili kujua kama huyu ni mnunuaji au polisi.