Pages

Sunday, 8 September 2013

Kibano chamgeukia Ndugai 



Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
*Yadaiwa alipewa maelekezo kuwabana wapinzani
*Profesa Lipumba adai uwezo wake bungeni mdogo

NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amezidi kujiweka katika wakati mgumu, baada ya viongozi wa vyama vya upinzani kudai alipewa maelekezo na Serikali kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba. Kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), walisema ni wazi, Ndugai ameonekana kuwa na uwezo mdogo wa kuongoza Bunge, kutokana na kusababisha vurugu kubwa ndani ya ukumbi wa Bunge wiki iliyopita.

Mtoto amkatakata mamaye kinyama

Na Lilian Mkusa, Njombe
WIKI iliyopita katika Mtaa wa Maheve uliopo Kata ya Ramadhani mkoani Njombe yalitokea mauaji ya kutisha yanayomhusisha mtoto aliyemkatakata mama yake mzazi kwa shoka kutokana na kugombania mirathi.

Wazanzibari waliumbua Bunge

Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal(kulia), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki mara baada ya kufungua Kongamano la Katiba Mpya na Nafasi ya Wazenjibara (Wazanzibari wanaoishi bara)

Makubwa zaidi yafichuka dawa za kulevya

Mhadhiri na Mtaalamu wa Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Kitila Mkumbo 
Kwa ufupi
Kwa yule ambaye si mzoefu wa kutumia vilevi hivi huwezi kuuziwa, kwani kuna ishara ambazo hupeana ili kujua kama huyu ni mnunuaji au polisi.

JK azindua shule, x-ray Mwanza

 

Mwanza. Rais Jakaya Kikwete amefungua shule ya kisasa ya msingi ya Ntulya Wilaya ya Misungwi, iliyotolewa zawadi kwa wanakijiji na taasisi kutoka Marekani.

Maelfu hatarini kukosa mtihani kidato cha nne 2013


Kwa ufupi
Tayari Necta imetuma barua kwa watahiniwa hao kuwaeleza kuwa hawatafanya mtihani mwaka huu.

Dar es Salaam. 

MWILI WA MWANAMKE ALIEUWAWA KIUKATILI KAWE JIJINI WASAFIRISHWA KWA MAZISHI MKOANI DODOMA


001.YustaMwili wa Marehemu Yusta Mkali ukiwa tayari kwa kuagwa Hospital ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam,na kuanza kwa safari ya mazishi yatakayofanyika kijiji cha Nzasa  Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma. 002.YustaBaadhi ya wafanyakazi aliokuwa akifanya nao kazi wakitoa heshima za mwisho
003.YustaWakinamama wakilia kwa uchungu
004.YustaMtoto wa Marehemu Baraka Simon(12)akimuaga mama yake mzazi kabla ya safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi kuanza aliemshikilia ni mama yake mkubwa Lucy Ngorido.
005.YustaJeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Yusta Mkali likifunikwa na kupandishwa kwenye gari tayari kwa kuanza safari ya kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi yatakayofanyika hapo kesho. 006.YustaSafari imeanza
007Mtuhumiwa Musa Senkando ambaye bado anatafutwa na Polisi kwa mahojiano wananchi tunaomba msaada wenu kwani huyu anadaiwa kuhusika na kifo cha mawanamke huyo