Pages

Thursday, 4 September 2014

UHARIBIFU WA MAZINGIRA MTO NZOVWE MBEYA WAKITHIRI

Wananchi waishio maeneo ya mwakibete mjini hapa wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria dhidi ya watu wanaofanya shughuli zao katika mto nzovwe kwani kufanya hivyo ni uharibifu wa chanzo hicho cha maji pamoja na kuhatarisha afya za watumiaji wengine wa mto huo.


Wakizungumza na mtandao huu wakazi hao wamesema kuwa baadhi ya wananchi huchimba mchanga, kufua kuoga pamoja na kuosha mboga za majani hali ambayo inahatalisha afya za kutokana na usalama wa maji hayo kuwa mdogo.

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kata hiyo RHODA NDINGANIA amesema kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakifanya jitihada za kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu mto huo lakini bado baadhi ya watu hawasikii na huendelea kufanya shughuli hizo.

Bi. NDINGANIA ametoa wito kwa watu hao kuacha mara moja kufanya shughuli hizo katika mto huo na kwamba atakayekaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Na Tegemea Ngabo- Mbeya.

No comments:

Post a Comment