Pages

Monday, 23 September 2013

JOHNSON JABIR MWANDISHI HABARI AVAMIWA, APIGWA NA MAPANGA, AJERUHIWA

ARUSHA: (JAIZMELALEO) - Maisha ni safari ndefu wadau wa JAIZMELALEO.
Siku zote mshukuru Mungu kwa kila jambo linapotokea katika maisha yako wala usiwe na hofu kabisa hata kama linauma kama nini LEAVE TO GOD.
Usiku wa kuamkia Septemba 22, 2013 katika mtaa wa Elkurei katika Kata ya Kiranyi, Arumeru mkoani Arusha wezi walinivamia na kunijeruhi haswa.
Walibeba vifaa vya kazi lakini kubwa zaidi ilikuwa ni kunitoa roho lakini Mwenyezi Mungu alininusuru kwa kunitia nguvu kupambana nao walikunja na marungu, visu na mapanga.
JINA LA BWANA LIBARIKIWE KWA YOTE.
Kwa niaba ya kikosi kazi cha mtandao wa www.kalulunga.blogspot.com ninatoa pole sana kwa ndugu yetu Johnson Jabir.
Mungu akuponye haraka na kumbuka kuwa kisasi ni juu ya Mungu.

No comments:

Post a Comment