Mchakato wa kumrejesha Alex Massawe waiva
mfanyabiashara maarufu Alex Massawe, anayetafutwa na vyombo vya usalama
Kwa ufupi
Hati hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Geni Dudu,
kufuatia maombi ya Jamhuri, yaliyotolewa na Wakili Mwandamizi wa
Serikali Tumaini Kweka, baada ya kumfungulia kesi ya jinai.
endelea.......
Dar es Salaam. Mchakato wa kumrejesha nchini, mfanyabiashara maarufu Alex Massawe, aliyekamatwa Dubai, Falme za Kiarabu, umeanza rasmi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa hati ya kumkamata na kumrejesha nchini kujibu mashtaka.
endelea.......
Dar es Salaam. Mchakato wa kumrejesha nchini, mfanyabiashara maarufu Alex Massawe, aliyekamatwa Dubai, Falme za Kiarabu, umeanza rasmi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoa hati ya kumkamata na kumrejesha nchini kujibu mashtaka.
Hati hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Geni
Dudu, kufuatia maombi ya Jamhuri, yaliyotolewa na Wakili Mwandamizi wa
Serikali Tumaini Kweka, baada ya kumfungulia kesi ya jinai.
Katika kesi hiyo namba 150 ya mwaka 2013, Massawe anakabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuwasilisha hati za nyumba.
Massawe ambaye alikamatwa hivi karibu na Shirika
la Kimataifa la Polisi (Interpol), amekuwa akitafutwa akihusishwa na
matukio ya uhalifu. Mahakama hiyo ilitoa usahihi wa majina yake, kuwa ni
Alex Siryamala Massawe.
Kwa mujibu wa Kweka, mtuhumiwa anayeshikiliwa
katika nchi nyingine anapoombwa kurejeshwa nchini,lazima kuwe na kesi
ambayo anatakiwa kujibu mashtaka, vinginevyo inaweza kuwa vigumu kwa
sababu inaonekana kuwa anatakiwa kwa masuala ya kisiasa.
Massawe alikamatwa kati ya Juni 20 na 25, mwaka
huu wakati wa ukaguzi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai,
kufuatia notisi ya Interpol walioombwa na polisi wa Tanzania kumnasa
mfanyabiashara huyo.
Siku chake baada ya kumnasa, Interpol lilimtangaza
mfanyabiashara huyo kwenye tovuti yake kama mtu anayetakiwa kukamatwa
na kurudishwa Tanzania kujibu tuhuma za uhalifu.
Utaratibu wa Interpol unaelekeza kuwa lazima
litolewe tangazo la mtuhumiwa kutakiwa kukamatwa na kurudishwa katika
nchi anayotuhumiwa kufanya makosa pale anaponaswa kwenye nchi ya kigeni.
Tangazo hilo kwa kawaida huwekwa picha, maelezo ya mtuhumiwa na alama nyekundu.
Taratibu za Interpol zinasema kuwa mtuhumiwa
anayewekewa alama nyekundu ni yule, ambaye anatakiwa kukamatwa na
kusafirishwa kwenye nchi anayotafutwa.
Hivyo katika tangazo hilo, lililowekwa kwenye
tovuti ya Interpol, picha ya Massawe pia iliwekewa alama hiyo nyekundu
kuashiria kuwa anatakiwa kurejeshwa nyumbani kutoka UAE.
Mbali na kesi hiyo, Massawe aliwahi kutajwa katika kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Onesphory Kituly.
No comments:
Post a Comment