Serikali, Tume ya Uchaguzi wavutana
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.PICHA|MAKTABA
Dar es Salaam. Wakati Serikali ikisema Daftari
la Kudumu la Wapigakura litaboreshwa kwa ajili ya kura za maoni ya
Katiba Mpya, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema haina mpango huo
kwa sababu muda uliobaki ni mfupi.
Badala yake Nec imesema inajiandaa kuboresha
daftari hilo kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili kuingiza wale wote waliotimiza miaka 18
baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.