WADAU WA NISHATI YA UMEME WA MAPOROMOKO YA MAJI NJOMBE WAAHIDI KUFANYA MAKUBWA BAADA YA MAFUNZO.
Pages
Thursday, 12 December 2013
Serikali, Tume ya Uchaguzi wavutana
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.PICHA|MAKTABA
Dar es Salaam. Wakati Serikali ikisema Daftari
la Kudumu la Wapigakura litaboreshwa kwa ajili ya kura za maoni ya
Katiba Mpya, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema haina mpango huo
kwa sababu muda uliobaki ni mfupi.
Badala yake Nec imesema inajiandaa kuboresha
daftari hilo kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 na
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili kuingiza wale wote waliotimiza miaka 18
baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
ANC walaani Zuma kuzomewa, wananchi wadai alistahili hilo
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma.PICHA|MAKTABA
Johannesburg.Chama Tawala cha Afrika Kusini,
Africa National Congress (ANC) kimekasirishwa na kuzomewa kwa Rais wa
nchi hiyo, Jacob Zuma wakati wa Ibada ya kitaifa ya heshima za mwisho
kwa rais wake wa kwanza mzalendo, Mzee Nelson Mandela.
Ni vilio vitupu A. Kusini
Mjane wa Rais wa Kwanza Mazalendo wa Afrika Kusini, Graca Machel akitoa
heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe katika Ikulu ya Pretoria nchini
humo jana. Picha na AFP
Pretoria: Familia ya Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini,
Nelson Mandela jana iliongoza utoaji wa heshima za mwisho kwa mwili wa
kiongozi huyo, katika tukio ambalo limebadili mwelekeo wa maombolezo
tangu alipofariki dunia, Desemba 5, mwaka huu.
Jeshi la Polisi Singida laua majambazi wawili
WADAU TUNAOMBA RADHI KWA TASWIRA HII KAMA ITAKUKWAZA.

WATU
wawili wakazi wa manispaa ya Singida ambao majina yao bado
hayajajulikana,wakiwa kwenye Jokofu la kuhifadhia maiti baada ya kuuawa
wakati wa majibishano ya risasi na polisi.(Picha na Nathaniel Limu).
Kamanda
wa polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela,akionyesha bunduki ya
kijeshi aina ya SMG no.34555 iliyokuwa ikitumiwa na watu wawili
wanaodhaniwa kuwa majamabazi katika kijiji cha Manga manispaa ya
Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Sunday, 8 December 2013
Subscribe to:
Comments (Atom)

