Baraza la Usalama laidhinisha azimio kuhusu Syria

Baraza
la usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio jana
Ijumaa(27.09.2013)ambalo linataka kuondolewa kabisa kwa silaha za sumu
nchini Syria lakini halitishii kuchukuliwa hatia za kuiadhibu serikali
ya rais Bashar al-Assad iwapo haitatekeleza.

