Kiama cha wauza unga chaja, faini kuondolewa, kifungo ni cha maisha
Madawa ya kulevya (Unga) yakiwa chini ya ulinzi
Kwa ufupi
Sheria iliyopo sasa ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya
ya mwaka 1995 (Sura ya 95, Ibara ya 16) inasema, endapo mtu atakamatwa
kwa kosa la kumiliki, kusafirisha, kuzalisha au kutengeneza mashine ya
dawa za kulevya, atahukumiwa kifungo cha maisha jela au kulipa faini ya
Sh10 milioni.

