
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
*Yadaiwa alipewa maelekezo kuwabana wapinzani
*Profesa Lipumba adai uwezo wake bungeni mdogoNAIBU
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amezidi kujiweka katika wakati
mgumu, baada ya viongozi wa vyama vya upinzani kudai alipewa maelekezo
na Serikali kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba.
Kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) na Chama cha Wananchi (CUF), walisema ni wazi,
Ndugai ameonekana kuwa na uwezo mdogo wa kuongoza Bunge, kutokana na
kusababisha vurugu kubwa ndani ya ukumbi wa Bunge wiki iliyopita.