Pages

Wednesday, 4 September 2013

Wabunge Chadema, CUF watoka nje

Kwa ufupi
  • Unashabikia mambo ya Tundu Lissu leo, endelea ila mtashughulikiwa,” aliunukuu ujumbe huo na kuongeza kuwa hafahamu umetoka kwa mbunge gani ila wahudumu wa Bunge ndio waliompelekea.

Dodoma.
Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni jana jioni walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kupuuzwa kwa mwongozo wao wa kutaka kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa.
Wabunge waliotoka bungeni jana yapata saa 12.15 ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi huku Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP, Augustine Mrema akiendelea kubaki ukumbini.
Kitendo cha wabunge hao wa upinzani kilionekana kuwakera baadhi ya wabunge wa CCM, ambao walisikika wakiwakejeli kwa kupiga meza huku wakisema: “Kwendeni zenu, tumewazoea.”
Wakati wabunge hao wakiondoka, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alikuwa akiwasisitiza wabunge wanaobakia wawe watulivu, maana kuna usalama wa kutosha ndani ya ukumbi huo.
“Mnaotoka nimewaona wote na mnanijua,” alisikika Naibu Spika Ndugai akiwatahadharisha wabunge wa upinzani waliosusa mjadala huo.
Wabunge wa CCM waliendeleza vituko ambapo baada ya wapinzani kutoka, wabunge Juma Nkamia (Kondoa Kusini), Hilary Aeshi ( Sumbawanga Mjini) na Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) walikwenda kukaa katika viti vya kambi ya upinzani.
Kabla ya kutoka kwa wabunge hao wabunge wawili kutoka CUF waliomba mwongozo wa Spika, wakitaka muswada huo kuondolewa ili kuwapa nafasi Wanzanzibar kutoa maoni yao.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohamed Mnyaa (CUF) aliomba mwongozo akitaka muswada huo uondolewe, hadi hapo Wazanzibar watakaposikilizwa.
Alisema kuwa kwa maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wamesikiliza maoni ya wadau wengi, lakini Zanzibar hawakwenda kuwasikiliza wadau wa eneo hilo.
“Na hili suala zima katika masuala ya katiba linahitaji usawa wa washirika, tunazungumza kitu kinachohusiana na Zanzibar na Tanzania Bara, ili kupata maoni ya nchi nzima kuna uhalali gani wa Bunge hili kuendelea na mjadala huu?” alihoji.
Hata hivyo, alikatizwa na kelele za Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), ambaye alitoa taarifa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilialika wajumbe mbalimbali ikiwamo Zanzibar.
“Miongoni wa wajumbe walioalikwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali ambao walikuja mbele ya Katiba,” alisema Pindi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.

Wananchi waHALMASHAURI YA BUSOKELO Wilaya ya RUNGWE Mkoani MBEYA wajadili rasimu ya Katiba katika mchakato unaoendelea nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi isiyokuwa ya kiraia inayojumuisha waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya inayojulikana kama ELIMISHA, kushoto  FESTO SIKAGONAMO amesema lengo ya asasi hiyo ni kuwapa fursa wananchi wa vijijini kuweza kutoa maoni yao katika mchakato wa Katiba

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA SUDAN

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali,kabla ya mazungumzo naye, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo.

Rwanda yajitetea kuhusu ushuru

 
Kwa ufupi
Ni ule wa kupandisha tozo za magari iliyopandishwa na nchi hiyo kwa madai ya kufanya ulinganifu

Dar es Salaam/Dodoma. Wakati ushuru wa magari makubwa ukiwa umeshushwa kwa wiki moja, Serikali ya Rwanda imejitetea ikisema haijafanya hujuma yoyote dhidi ya Tanzania, bali imepandisha tozo hiyo ili kuifanya ilingane na ile inayolipwa Tanzania.

Mahakama yaruka shutuma kuwaachia washtakiwa dawa za kulevya ‘kiaina’

 
Kwa ufupi
  • Akizungumza na waandishi wa habari jana, ofisini kwake, Jaji Jundu alikanusha tuhuma hizo akisema kuwa majaji na mahakimu wamekuwa wakitoa uamuzi kwa kuzingatia ushahidi na misingi ya kisheria.

Kibanda, Mwigamba wajitetea


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Tido Mhando (katikati), akifurahia jambo na Meneja Uendelezaji Biashara, Theophil Makunga na Mwanasheria MCL, Doris Marealle nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, kabla ya kuanza kwa kesi ya uchochezi inayomkabili Makunga na wenzake wawili.

‘Mvua za Lowassa’ zagonganisha mawaziri

 


  • Malumbano hayo yalisababishwa na swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo ambaye alihoji mpango wa kutengeneza mvua ulipoishia kwa kuwa Serikali imekuwa kimya.