Kumekucha Uchaguzi Mkuu 2015, Lowassa atikisa CCM, upinzani
viongozi wa vyama na Serikali nchini Tanzania ambao majina yao yanatajwa
na wananchi kuwa wanaweza kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu
mwakani.
Kwa ufupi
Wakati Lowassa angeibuka na ushindi kwa asilimia 13
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda angefuatia kwa karibu akiwa na asilimia 12
huku Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiwa wa tatu kwa
asilimia kumi na moja.
Wakati Lowassa angeibuka na ushindi kwa asilimia
13 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda angefuatia kwa karibu akiwa na asilimia
12 huku Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiwa wa tatu kwa
asilimia kumi na moja.
Hata hivyo, asilimia 33 ya wananchi waliohojiwa walisema bado hawajaamua wampigie kura mgombea gani.
Utafiti huo wa Taasisi ya Twaweza unayoonyesha
wagombea hao kukabana kwa tofauti ya asilimia mojamoja na ambao
ulitangazwa Dar es Salaam jana, ulifanywa Septemba 2014 kwa kuwahoji
wananchi 1,445 kutoka Tanzania Bara.
Akitangaza matokeo hayo, mtafiti wa Twaweza, Elvis
Mushi alisema utafiti huo ni wa tatu kufanyika nchini na kwamba awamu
ya kwanza ilifanyika mwaka 2012 na Lowassa alipata asilimia sita kabla
ya mwaka jana na mwaka huu kuibuka na asilimia 13.
Akimzungumzia Pinda, mtafiti huyo alisema mwaka
2012 alipata 16, lakini zilishuka mwaka 2013 hadi kufikia asilimia kumi
na moja na kupanda tena mwaka huu hadi 12.
“Kwa upande wa Dk Slaa, mwaka 2012 na 2013 alipata asilimia 19 lakini sasa ameshuka hadi asilimia kumi na moja,” alisema Mushi.
Wagombea wengine waliotajwa na asilimia zao kwenye
mabano ni Profesa Ibrahim Lipumba (6%), Dk John Magufuli (3%), Freeman
Mbowe (3%), Samuel Sitta (4%), Bernard Membe (5%) na Zitto Kabwe (1%).
“Hata hivyo, kitu muhimu cha kuangalia katika
ripoti hii siyo tu majina ya mgombea, bali ni idadi ya wananchi asilimia
33 ambao wamesema hawajui watamchagua nani,” aliongeza Mushi.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa iwapo vyama vyote vya
upinzani vitaungana na kumchagua mgombea urais mmoja, asilimia 41 ya
wananchi waliohojiwa walisema wangemchagua Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Willibrod Slaa, akifuatiwa na Profesa Lipumba (14%), Mbowe (11%) na
Zitto Kabwe (6%).
Wanasiasa wengine waliotajwa ni Tundu Lissu,
Maalim Seif Sharif Hamad, James Mbatia na Augustino Mrema ambao kila
mmoja aliambulia asilimia moja.
Wengi kuchagua CCM
No comments:
Post a Comment