Pages

Monday, 21 July 2014

newwwws

Chadema ngangari, yasisitiza kutoshiriki Bunge la Katiba



  • Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salam jana, kuhusu maazimio ya Kamati Kuu ya Chama hicho, iliyokutana kwa siku mbili Dar es Salaam, Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa. Picha na Venance Nestor 

Dar/Zanzibar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema wajumbe wa Bunge la Katiba kutoka katika chama chake hawatashiriki katika Bunge hilo linalotarajiwa kuendelea mwezi ujao.
Aidha, amesema Chadema haitashiriki katika kikao cha Julai 24 kilichoitishwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta akisema hicho ni sehemu ya Bunge hilo ambalo wajumbe wake na wenzao wanaounda Umoja wa Katiba ya Watanzania (Ukawa) walilisusia.
Akisoma tamko la Kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alisema iwapo Bunge hilo litapitisha Rasimu ya Katiba Mpya isiyotokana na maoni ya wananchi, chama hicho kikiwa sehemu ya Ukawa, kitafanya kampeni nchi nzima kuwashawishi wananchi kuikataa wakati wa upigaji wa kura ya maoni.
Alisema kuliko kupata Katiba Mpya ambayo ni mbovu ni bora mchakato wa kuipata uchelewe ili Ukawa waendelee kupigania Katiba bora itakayopatikana kutokana na maoni ya wananchi na siyo maoni ya CCM.
Wakati Mbowe akieleza hayo, CCM Zanzibar kimeibuka na kutaka Ukawa kuacha visingizio na badala yake waungane na wabunge wengine kujadili na kupitisha Rasimu ya Katiba bila ya kutoa masharti.
Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu alisema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa nyumba kumi, mashina, matawi, wadi na jimbo huko Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema siyo busara kwa wabunge wa Ukawa kutoa visingizio visivyo na mashiko na kutozingatia masilahi ya umma na tija ya kupatikana kwa Katiba Mpya ijayo mwaka 2015.
Mambo manne

No comments:

Post a Comment