Marubani wageni ‘wavamia’ soko la ajira Tanzania

Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imesema ajira ya marubani wazalendo
ipo mashakani kwa sababu ndege nyingi nchini, zinaongozwa na wageni.TCAA
imesema hali hiyo imekuwa ikichangiwa na kampuni zinazotoa huduma hizo
nchini, kutumia ndege nyingi za kukodi zinazofanya kazi chini ya
masharti yanayotoa nafasi kubwa ya kuongozwa na marubani wa kigeni.(hd)
"Ndege ni
ghali sana na wengi walioko kwenye sekta hii wanakopeshwa na kupewa
masharti,"alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhili Manongi, alipokuwa
akizungumza katika mahojiano na gazeti hili.
Alisema karibu asilimia 50 ya marubani wanaoendesha ndege zinazofanya kazi hapa nchini, ni wa kigeni.
Manongi alisema ingawa mikataba kuwabana, kigezo cha uzoefu pia ni kikwazo kwa marubani wengi wazalendo.
"Wengine wanashindwa kupata ajira kutokana na kutokuwa na saa zinazohitajika ili mtu aweze kurusha ndege za biashara," alisema.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, kwa sasa Tanzania ina marubani 500 na katika miaka mitatu ijayo watafikia 700.
Alisema
kwa jumla sekta ya usafiri wa anga ina upungufu wa wataalamu kama
wahandisi na marubani lakini shida kubwa inawahusu zaidi marubani.
Manongi
alisema kwa kuzingatia hali hiyo, TCAA ipo kwenye mikakati ya kuboresha
sekta ya marubaini nchini ili pamoja na mafunzo, pia wapate uzoefu
utakaowawezesha kutoa ushindani kwenye soko la ajira ndani na nje ya
nchi.
No comments:
Post a Comment