Pages

Saturday, 28 September 2013

Hassan Sheikh Mohamud; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu.


shehki_871e3.jpg
Ni Rais wa Somalia. Kwa hakika, kwa sasa ndiye Rais wa nchi ya Kiafrika mwenye wakati mgumu sana. Na katika shida zake, Hassan Sheikh Mohamud ameonekana, si mara moja, akitua Dar Es Salaam, kwenye Ikulu ya JK. Kwa Hassan Sheikh Mohamud aliye matatizoni, kufunga safari ya Dar kwa JK ni kama kwenda kwa Obama! Kuna tofauti kubwa na Mogadishu.

Kiukweli Hassan Sheikh Mohamud hana eneo kubwa la nchi ambalo anaweza kusema kuwa analidhibiti. Kuna wakati ikasemwa, kuwa anadhibiti maeneo jirani tu na Ikulu yake ya Mogadishu. Huko kwengine kuna ' Mabwana wa Vita'.
Na sasa ni ' pasua' kichwa ya Al shabaab. Tofauti na inavyoonekana nje, Al shaabab hawajawa na nguvu za kutisha sana. Isipokuwa, wakiachwa wakue, ni ' pasua' kichwa si tu kwa Somalia, bali kwa nchi zetu hizi.(P.T)

Shambulizi la Wastgate ni ishara za Al Shabaab wanaoanza kuota mapembe. Kuna mantiki ya Marais wa nchi jirani na Somalia ikiwamo Tanzania, chini ya mwevuli wa AU na UN, kufanya jitihada za kuungana katika kupanga mikakati ya kumsaidia Hassan Sheikh Mohamud.
Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab, ambayo kimsingi.



No comments:

Post a Comment