Kodi kuhamisha fedha yapingwa
Benki kuu ya Tanzania(BOT)
- Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyochapishwa kwenye magazeti jana, chama hicho kimesema kuwa hakikushirikishwa katika utungaji wa sheria hiyo bali kilipata taarifa kupitia mawasiliano yake na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa mujibu wa sheria hiyo ambayo haikuwepo kwenye
hotuba ya bajeti wala kujumuishwa kwenye muswada wa fedha, kutakuwa na
ushuru kwa uhamishaji wa fedha kupitia benki, taasisi ya fedha au
kampuni ya mawasiliano ya simu kwa kiwango cha asilimia 0.15 kwa kiwango
kisichozidi Sh30,000.
Katika taarifa yao kwa vyombo vya habari
iliyochapishwa kwenye magazeti jana, chama hicho kimesema kuwa
hakikushirikishwa katika utungaji wa sheria hiyo bali kilipata taarifa
kupitia mawasiliano yake na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Msimamo huo umekuja ikiwa ni siku chache tangu
wadau wa sekta ya mawasiliano kupinga kodi ya kadi za simu ambapo kila
mwananchi alitakiwa kukatwa Sh1,000 kwa mwezi.
Alipoulizwa kuhusu msimamo huo wa TBA, Naibu
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum licha ya kusita kuzungumzia
alishangazwa na mtindo wa kupinga kodi tangu ile ya kadi za simu ambayo
pia ilipitishwa katika Bunge la Bajeti la mwaka huu.
No comments:
Post a Comment