Kamati kuu ya CCM kuamua hatma ya Madiwani Bukoba.
Halmashauri
Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku
moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia
dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya
Bukoba waliotokana na CCM.
endelea.....
Kwa
mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye
vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya
Mkoa sio wa mwisho. Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.
Hivyo
basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa
kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini
Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa
Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.
Pamoja
na hilo, tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi
huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa
utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
Tunawasihi
wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa
watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao
vya Kitaifa.
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
14/08/2013

No comments:
Post a Comment