Pages

Tuesday, 6 August 2013


38 wafa kwa mafuriko Sudan

Wananchi wakiwa juu ya maji baada ya kutokea mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha na kusababisha vifo vya watu 30. (PICHA NA FOXNEWS)

KHARTOUM, Sudan
WATU wasiopungua 38 wanaripotiwa kupoteza maisha nchini Sudan baada ya kutokea mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko.

endelea
Watu hao wamekufa kutokana na matukio mbalimbali yaliyosababishwa na mafuriko yakiwemo kubomoka nyumba zao, kusombwa na maji au kupigwa na shoti ya umeme.   Aidha janga limesababisha maelfu ya nyumba kubomoka na hivyo kuwaacha bila makazi watu wengi wa maeneo ya kaskazini katika Jimbo la Darfur.   Maelfu ya familia  katika maeneo ya mashariki zinakabiliwa na hali mbaya huku nyumba zao zikiwa zimesombwa na mafuriko hayo.
Waathiriwa wa mafuriko hayo wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula huku wakihitaji misaada ya kitiba.
Tayari Serikali ya Sudan imeanza kupeleka misaada ya kibinadamu katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hayo.

No comments:

Post a Comment