Mtei: Tutaendelea kuwafukuza wasaliti
Mwasisi wa Chadema Edwin Mtei anamtaka Saidi Arfi aache kulalamika kwani
“kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa mwenyekiti wa Chadema
taifa alipaswa kujichunguza kwanza.” PICHA | MAKTABA
Arusha. Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwafukuza wote wanaokihujumu huku akieleza kwamba, anaunga mkono kuvuliwa uongozi kwa Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.

