Pages

Sunday, 1 September 2013

Mauaji ya kutisha mkoani Simiyu

Wakazi wa Simiyu wakiwa katika moja ya mikutano yao
Kwa ufupi
Taarifa zinaonyesha kuwa kwa mwaka jana pekee, wastani wa watu watatu walikuwa wakiuawa kila wiki na kikundi hicho cha watu kinachofahamika kama Baraza la Kimila katika Mkoa wa Simiyu, wakiwamo wanawake na watoto.

Bastola nje nje, zauzwa mitaani nchini

  
  Kwa ufupi
Uchunguzi wa kina wa gazeti hili katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo iliyopo mipakani inaonyesha kuwa, bastola zinamilikiwa na watu bila ya kufuata taratibu na nyingine zikitumika kwa ajili ya kufanyia uhalifu.


Friday, 30 August 2013

Wanawake wataka Katiba iainishe usawa

Baraza la Kitaasisi la Wanawake Wanahabari, limesema Katiba mpya iainishe suala la usawa katika nyanja zote za uongozi ikiwa ni pamoja na uongozi wa mihimili mikuu mitatu ya utawala yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa kujadili masuala muhimu ya kijinsia yanayopaswa kuingizwa katika rasimu ya Katiba mpya uliofanyika jana jijini Dar es Salaam, wajumbe wa baraza hilo walitaka Katiba mpya izingatie zaidi fursa katika usawa wa uongozi na kutolea mfano kuwa kama mwanaume atakuwa waziri basi katibu mkuu awe mwanamke na siyo kupewa nafasi ya usaidizi.

"Licha ya rasimu kuainisha haki za wanawake katika ibara ya 46, lakini bado kifungu cha 1 (c) hakimpi nafasi mwanamke kushiriki kikamilifu katika chaguzi za ngazi zote za maamuzi na uongozi, hivyo kuwepo na mazingira wezeshi," alisema Mratibu wa taasisi ya wanawake ya Ulingo, Avemaria Semakafu. 

Semakafu alisema katiba iweke na chombo maalum cha kusimamia haki za watoto na wanawake kwa kuwa rasimu haijaonyesha, hivyo kwa kuzingatia suala hilo utaratibu utawekwa wa kuunda tume itakayosimamia na kuhakikisha viongozi na wananchi katika ngazi zote wanaitekeleza ibara hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini (Tamwa), Valerie Msoka alisema Katiba itaje umri kamili wa mtoto na muda rasmi wa kuruhusiwa kuoa au kuolewa. 

Pia alitaka itaje kiwango cha haki ya elimu kuwa mpaka kidato cha nne pamoja na kutoa mazingira rafiki ya kumwezesha watoto wa kike kupata elimu kwa usalama zaidi.

Kwa upande wake, mjumbe kutoka Mtandao wa Mashirika ya Haki za Binadamu Kusini mwa Afrika, Matrina Kabisana alisema rasimu haijatoa haki ya kuishi kwa asilimia 100, kwani bado haijaweka kipengele cha kukataza adhabu ya kunyongwa mpaka kufa (kifo).

CCM KUWASAIDIA WAZEE

 Baadhi ya wawakilishi wa Mtandao wa Wazee wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye nje ya ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma leo tarehe 30 Agosti 2013.

WAASI WA M23 WAMUUA MWANAJESHI WETU WA JWTZ HUKO KONGO


TAARIFA KUHUSU TUKIO LA KUFARIKI KWA AFISA WA JWTZ KATIKA JUKUMU LA KULINDA AMANI - DRC, GOMA

Majambazi yapora Sh900 milioni benki asubuhi

Suleiman Kova 
Kwa ufupi
  • Alisema mmoja wa majambazi hao alikuwa ni mtu mwenye asili ya Asia na kwamba walikuwa wakizungumza Kiingereza kuwasiliana.

Saa 4 zawatenganisha pacha walioungana

Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Muhimbili, Profesa Karim Manji (wa pili kushoto) akifurahia na wenzake baada ya kufanikiwa kwa operesheni ya kuwatenganisha watoto walioungana, kazi iliyofanywa na jopo la madaktari bingwa saba kwa saa 4.